Papa Francisko akutana na tume kwa ajili ya tuzo ya Zayed ya Udugu wa ubinadamu!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Tume ya majaji wa kwa ajili ya Tuzo ya Zayed ya Udugu wa ubinadamu wamekutana na Papa Francisko kwa mara ya kwanza tarehe 23 Oktoba 2020. Fursa hiyo ilikuwa ni katika kikao cha kufanya kazi kilichopangwa huko Roma ili kujadili mifumo ya tathmini ambayo majaji hao watafuata hadi kutangazwa kwa mshindi mnamo Januari 2021. Katika mchakato wa mkutano wao, wametoa fursa ya kuteua mtu maalum na taasisi ambazo zimetoa mchango mkubwa kwa ajili ya ubinadamu
Jumatatu, tarehe 19 Oktoba, (HCHF) chombo hiki kilitangaza wito wa maombi ya duru ya pili ya tuzo na ni kwa mara ya kwanza hii kutokea. Katika kikao cha ufunguzi, utambuzi huo uliwaendelea Imam Mkuu wa Al-Azhar, Al-Sharif, profesa., Ahmed Al-Tayyeb, na Na Papa Francisko kutokana na jukumu lao katika kusaini Hati juu ya Udugu wa Binadamu (DHF) huko Abu Dhabi, Februari 2019.
Wajumbe wa Tume hiyo ya kuandaa Tuzo ya Zayed ya Udugu wa Binadamu waliipongeza Hati hiyo (DHF), wakionyesha umuhimu wake kwa wanadamu wote, hasa kwa kuzingatia changamoto na shida ambazo ulimwengu unapitia. Walitoa pongezi pia juhudi zilizofanywa na tuzo ya udugu wa kibinadamu (HCHF) kukuza utamaduni wa kuishi pamoja, na pia mpango wa kuunga mkono tuzo na kuweka vigezo katika tuzo yake. Tume hiyo ya majaji ilionyesha shukrani zao kwa utayari wa UAE kuunga mkono juhudi za kufikia malengo ya DHF.