Tafuta

Maisha ya Carlo Acutis:Kipaji maalum cha Internet kwa ajili ya Uinjilishaji!

Katika Duka la vitabu la Vatican,wamewakilisha kitabu kipya kiitwacho kipaji maalum cha inteneti ambacho kinaelezea maisha ya Carlo Acutis.Utangulizi wa kitabu hicho ni Monsinyo Dario Viganò, Mshauri wa Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya sayansi na ya Sayansi Jamii. Mtumishi wa Mungu Carlo Acutis anatangazwa kuwa mwenyeheri,Jumamosi tarehe 10 Oktoba mjini Assisi.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Maisha ya Carlo Acutis katika kipaji maalum cha inteneti mbinguni, ni kitabu ambacho kimetolewa na Duka la Vitabu Vatican (LEV) kwa kutiwa sahini Nicola  Gori. Siku hizi ulimwenguni kote unazungumzia kuhusu kijana huyo Carlo Acutis, msimamizi wa Interneti ambaye ameweza kuunganisha maisha yake ya ujana katika sala na upendo mkuu wa Mama Maria na Ekaristi Takatifu. Ni katika fursa ya tarehe 10 Oktoba 2020 ambapo anatangazwa kuwa mwenyeheri. Mwaka 2016 Duka la Vitabu Vatican LEV lilikuwa limekwisha toa kitabu hivho  “Mwenye kipaji maalum cha  Internet mbinguni:Historia ya Mtumishi wa Mungu Carlo Acutis” kikiwa na  sahini ya Nicola Gori, ambaye ni msimamizi wa mchakato wa kutangazwa kuwa mwenyeheri. Kitabu hicho kinajumuisha historia ya kijana  huyo Carlo mwenye umri wa miaka 15 ambaye alikuwa alipenda Inteneti kama walivyo vijana wote wa rkca lake. Licha ya ujana wake huo Carlo Acutis anaamini kwamba mtandao unaweza kuwa gari la uinjilishaji na katekesi, yeye mwenyewe aliweka nguvu zake na uwezo wake wote kwenye mtandao katika huduma ya Injili na ya Kanisa kwa kupeleka Yesu kwa njia ya Intenet na mitandao ya kijamii kati ya rafiki zake na rika lake na wale wote ambao waliwasiliana na yeye.

Kati ya mambo yaliyo na upeo mkubwa wa maisha yake ni upendo mkuu kwa Bikira Maria na Ekaristi ya kila siku, kwa maana hakukosa hata siku moja kuudhuria misa na kuabudu. Inashangaza sana Mama yake anapoeleza kwamba kila mara walipokuwa wakitaka kwenda likizo, kitu cha kwanza aliulizia hilo eneo kama kuna Kanisa. Mama yake alifanya kila njia hasimkosesha hiyo ratiba yake mtoto wake. Wengi watamkumbuka sana kwa sentesi yake  semayo “L’Eucaristia è la mia autostrada per il cielo’’ yaani  “Ekaristi ni njia yangu ya kwenda mbinguni’. Yote hayo yamewekwa kwenye  mkanda (DVD) ambayo inasindikiza kwa muziki kitabu hicho.  Hata hivyo pia kuna sentensi moja ambaye inakumbukwa na wengi kwamba:isemayo: “Tutti nasciamo come degli originali, ma molti muoiono come fotocopie” yaani “Sisi sote huzaliwa kama asili, lakini wengi hufa kama nakala”. Upendo kwa Mungu na watu ni mambo yanayokimbia pamoja kwa furaha na kweli, alikuwa nasisitiza Carlo. Utangulizi wa kitabu hicho umetolewa na  Monsinyo Dario Viganò, Mshauri wa Taasisi ya Kipapa ya Elimu na Taasisi ya Kipapa Elimu ya Sayansi Jamii.

Hata hivyo ikumbukwe kwamba katika Wosia wa Kitume wa Christus Vivit, Carlo Acutis Papa anamtaja kijana huo kuwa ni wa wakati wake ambapo amejitahidi kutangaza Injili. Alitumia njia mpya za kiteknolojia hata kutrengeneza mpango wa maonyesho ya mijizi ya Ekaristi na ambayo inaendelea kuzunguka ulimwengu mziki, na kwa kipinid hiki maonyesho hayo yamewekwa mjini Asisi. Mama yake Antonia Salzano, amezungumzia sana juu ya mtoto wake alivyokuwa akicheza michezo ya kisayansi kwenye interne na kutengeneza video kwa kutumia camera yake na hata kutengeneza magazeti kwa kutumia progam maalum, tayaratibu alianza kujifunza mwenyewe matumizi yake yake na kwa maana hiyo kwa kujifunza yeye mwenyewe aliweza kuwa mtaalam sana.

Kwa mujibu wa Monsinyo Vigano anasema hii kiukweli ni zawadi. Zawadi ambaye ameiwkew kwa ajili ya huduma ya wema. Kwa mfano maonyeshi ya Miujiza ya Ekaristi imesafiri mamilioni ya parokia katika mabara kwa ajili ya kuimarisha imani kwa walio wengi ambao hawakuwa wanajua mafundisho halisi ya uwepo halisi wa Yesu katika Ekaristi. Haya ni mambo ambayo katika historia kweli yanaweza kuweka ndani ya moyo na zaidi kuwa na  mtazamo wa vijana wengi kwa kuwaelezea kwamba kuna  uwezekano leo hii kuishi uzoefu wa Injili. Haishangazi kuona kwamba katika historia hii, kwa haraka kumeendelezwa aina nyingi za mipago ya simulizi na vitab vingi ambavyo vinaelezea ukweli huo.

Iikimbukwe mtumidhi wa mungu Carlo Acutis Carlo, alizaliwa London, Uingereza  mnamo 1991, ambapo wazazi wake walikuwa huko  kwa sababu za kazi, alikuwa na utauwa wa kina wa  mapema sana . Alipokea Komunyo yake ya Kwanza, kwa idhini maalum, akiwa na umri wa miaka saba tu. Alikuwa kijana aliyeudhuria Misa kila siku na kusali  Rozari. Aliendelea kukua na upendo wa kupendeza kwa watakatifu, na kwa Ekaristi, hadi kufikia hatua ya kuanzisha maonyesho ya miujiza ya Ekaristi ambayo imebaki mtandaono hadi leo hii na imekuwa na mafanikio yasiyotarajiwa, hata nje ya nchi kwa ujumla ulimwenguni kote. Carlo alifariki dunia tarehe 12 Oktoba, 2006 na kifo chake kilitokana na ugonjwa wa Saratani ya damu (Leukemia) katika Hospitali ya Mtakatifu Gerardo, mji wa Monza, Italia. Mchakato wake wa kutangazwa mtakatifu ulipata kibali tarehe 13 Mei, 2013. Papa Francisko tarehe 5 Julai, 2018 alimtangaza kuwa Mtumishi wa Mungu. Na tarehe 21 Februari, 2020 Papa Francisko aliridhia mchakato wa kutangazwa kuwa MwenyeHeri. Na muuujiza unaomwinua kuwa Mwenye heri ulitokea kutokana na uponyaji wa mtoto chini Brazil aliyekuwa na shida ya kongosho hapo mwaka 2013. Jumamosi tarehe 10 Oktoba 2020 katika mji wa Assisi, Mtumishi wa Mungu Carlo Acutis atatangazwa mwenyeheri. Kwa habari zaidi soma ingia Vatican News.

https://www.vaticannews.va/it/chiesa/news/2020-10/carlo-acutisgenio-informatica-in-cielo-vangelo-web.html

https://youtu.be/31mENCFa5hk

09 October 2020, 15:22