Tafuta

2020.10.28 Kardinali  Anthony Soter Fernandez, Askofu Mkuu mstaafu wa  Kuala Lumpur, Malaysia. 2020.10.28 Kardinali Anthony Soter Fernandez, Askofu Mkuu mstaafu wa Kuala Lumpur, Malaysia. 

Kardinali Soter Fernandez wa kwanza nchini Malaysia amefariki

Kwa asili ni kutoka India,Kardinali Fernandez alikuwa miongoni mwa wahusika wakuu wa sasisho la kihistoria la 1976,wakati maaskofu wote na makuhani wa Malaysia walipokusanyika kwa mara ya kwanza kufafanua mpango wa kichungaji kwa kuzingatia Mtaguso wa Vatican II.Mazishi yataadhimishwa Jumamosi tarehe 31 Oktoba katika Kanisa Kuu la Kuala Lampur ambapo mwili wake utaonyeshwa.

Amefariki mapema kabla ya muda mfupi kuamkia siku ya Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 , Kardinali Anthony Soter Fernandez, Askofu Mkuu Mstafu wa Kuala Lumpur, kutokana na ugonjwa wa saratani ya ulimi iliyokuwa imempata kwa takriban mwaka mmoja. Alikuwa katika nyumba ya wazee  ya Mtakatifu Francisko wa Xaveri akihudumiwa na Watawa wa shirika la Dada wa Maskini huko Cheras. Hali yake ilikuwa imezidi kuwa mbaya katika masaa machache yaliyopita na Jumanne alipokea sakramenti ya upako wa wagonjwa. Kardinali ni mzaliwa wa familia yenye asili ya India mnamo tarehe 22 Aprili, 1932, katika eneo la jimbo la  Penang, huko Sungai Petani, karibu kilomita mia tatu kutoka mji mkuu wa Malaysia Kuala Lumpur.

28 October 2020, 15:46