Kardinalo Pietro Parolin,Katibu wa Vatican Kardinalo Pietro Parolin,Katibu wa Vatican  

Kard.Parolin:Lazima kuelimisha kujali ili kuongoza uchumi na siasa

Katika mkutano wa kimataifa kuhusu “hatua muhimu za ekolojia fungamani ya Uchumi wa Binadamu",iliyoandaliwa kwa njia ya mtandao na Mfuko wa Centesimus Annus pro Pontifice,KardinaliParolin Katibu wa vatican kwa njia ya video amejikita katika mada msingi ya Laudato si akiunganisha na Waraka wa Fratelli tutti.Mwaliko ni kuanzisha tena mfano wa maendeleo na ukuaji ambao unaweka katikati hadhi ya binadamu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika mwaka maalum ambao Papa  Francisko amependelea kujikika katika sala, tafakari na mazoea mazuri yanayoongozwa na Waraka wa Laudato Si ',  Mfuko wa Kipapa unaojulikanao kama “Centesimus Annus Pro Pontifice umeandaa mkutano wa kimataifa katika vikao viwili kwa mada mbili, ya kwanza ni “Mfano wa Utawala na Biashara” (tarehe 23 Oktoba) na wa pili unahusu “Elimu na Mafunzo” (tarehe 30 Oktoba).  Mikutano yote miwili inafanyika kwa njia ya mtanoa na kwenye jukwaa la Zoom, ikizingatiwa  dharura wa Covid-19. Aliyefungua Mkutano huo ni Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, kupitia ujumbe kwa njia ya video  mahali ambapo ameweza kuunganisha pamoja nyaraka mbili za Laudato Si 'na Fratelli tutti.

Kupokea wakati huu wa jaribio kama wakati wa uamuzi ulikuwa mwaliko wa Papa  Francisko kwa wakati  wa sala ya ulimwengu ambayo iliinua kwa Mungu, katika hatua kali ya janga hilo, katika Uwanja wa Mtakatifu Pero mnamo Machi 27 iliyopita. Kutokana  kwa maneno haya, amenukuu hotuba hiyo ambayo ilibaki kukumbukwa na pia kutoka kwa maandishi ya Fratelli, ambayo Papapa anatukumbusha kwamba janga hilo limetuweka wazi kiukweli juu ya uwongo wetu na kutulazimisha kukabiliana na udhaifu ya viumbe wa mwisho, amesema Kardinali Parolin.

Kardinali Parolin amerudi kuelezea kwamba dhana ya 'ekolojia fungamani inakwenda mbali zaidi ya mwelekeo wa 'mazingira  ikitutaka kuwa na maono zaidi fungamani  yenye mambo mengi ya maisha, ambayo huchochea sera bora, viashiria, michakato ya utafiti. na vigezo vya maendeleo na tathmini, kuepuka tafsiri potofu za ni nini maana maendeleo na ukuaji Umuhimu wa mwanadamu na hitaji la kukuza utamaduni wa utunzaji, kinyume na utamaduni wa taka: hii ndiyo kitovu cha njia hii ya maisha na usimamizi wa rasilimali.

Kuna haja ya utambuzi wa maadili kwa kupendelea tafakari mpya na ya kina juu ya maana ya uchumi na malengo yake, na vile vile marekebisho ya kina na ya kuona mbali ya mtindo wa maendeleo, ili kurekebisha shida zake na upotovu . Na kwa kwa wajasiriamali kardinali amesema vitendo vyao vinapaswa kuelekezwa wazi kwa maendeleo ya watu wengine na kushinda taabu, hasa kupitia kuunda fursa za ajira mbalimbali. Kardinali Parolin anasisitiza juu ya umuhimu kwamba uchumi wa binadamu unategemea jukumu la msingi la kazi ambalo anakumbuka katika jamii iliyoendelea kweli ni mwelekeo muhimu wa maisha ya kijamii, kwa sababu sio tu njia ya kupata mkate wa mtu, bali pia njia ya ukuaji binafsi, kuanzisha uhusiano mzuri, kujieleza, kushirikisha zawadi, kuhisi kuwajibika ili  kuboresha ulimwengu na hatimaye  kuishi kama watu. 

23 October 2020, 15:45