2020.09.07 "TerraFutura" - Ni jina la kitabu kipya ambacho kinahusu mazungumzo ya Papa Francsiko kuhusu Ekolojia Fungamani kilichoandikiwa na Carlo Petrini 2020.09.07 "TerraFutura" - Ni jina la kitabu kipya ambacho kinahusu mazungumzo ya Papa Francsiko kuhusu Ekolojia Fungamani kilichoandikiwa na Carlo Petrini 

TerraFutura:Mazungumzo na Papa juu ya ekolojia fungamani

"TerraFutura" ni jina la kitabu kipya ambacho kinahusu mazungumzo na Papa Francisko kuhusu Ekolojia Fungamani kilichoandikwa na Carlo Petrini.Ni tunda la mikutano ya Papa na mwandishi huyo wa masuala ya vyakula.Katika kitabu Papa Francisko anasimulia uongofu wa kiekolojia,kwani anathibitisha kwamba ikiwa tunataka kuwa na siku bora zijazo tunahitaji kubadilisha dhana zetu haraka.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Kitabu kipya kitolewa kilichoandikwa na aliyekuwa mkomunisti wa zamani na anayehusiana na masuala ya vyakula aitwaye Carlo Petrini, mwanzilishi wa “Slow food” akijikita kutazama mawazo ya Papa Francisko kwenye Waraka wake wa Laudato si. Katika mawazo yake akihojiwa na Vatican News anasema Papa, kama Francisko, ambaye kama Kardinali hakuelewa nguvu ambayo maaskofu wa Brazil walizungumzia juu ya shida kubwa za Amazonia katika mkutano wa Aparecida na wala nini kinachohusiana na jukumu lake kama askofu kuhusu afya ya mapafu ya kijani ya ulimwengu, ndiye baadaye aliweze kumshangaza kwa wosia huo maalum wa kujali na tahamani ya kutunza nyumba yetu ya pamoja.

Hata hivyo Mwandishi wa kitabu, Petrini na Papa wameunganishwa na mzizi mmojawa asili kwani wote asili yao ni kutoka Mkoa wa Piedmonte nchini Italia.  Akifafanua zaidi amesema kutokana kuwa mkutano wao ndipo kimezaliwa kitabu kiitwacho “TerraFutura” yaani dunia ya baadaye. Katika kitabu hicho ni mazungumzo yake na Papa Francisko juu ya ekolojia fungamani. Ni kitabu ambacho kitatolewa kwenye maduka ya vitabu tarehe 9 Septemba 2020 ambapo mwandishi wake Petrini pia ni mmoja wa wahamasishaji wa mtandao wa kimataifa wa Ekolojia uitwao “Madre Terra” yaani “Dunia Mama”.

Katika kufafanua Petrini anasema kuwa katika mazungumzo ya kwanza, mnamo tarehe 30 Mei,2018, miaka mitatu baada ya kuchapishwa kwa Waraka wa Laudato Si na ambapo ugeni huu Carlo anaufafanua kuwa ulikuwa kama  nguvu isiyo ya kawaida, ambayo "ilibadilisha hali ya mazungumzo ya kiekolojia na kijamii", kwani Papa Francisko alizungumzia juu ya mwanzo wa Laudato si’. Yeye katika mazungumzo hayo alikumbuka kuwa ni matokeo ya kazi ya watu wengi, wanasayansi, wataalimungu na wanafalsafa, ambao walimsaidia sana kufafanua kwa uwazi na ambapo zana zao zilifanya kazi kubwa juu ya muundo wa mwisho wa maandishi ya waraka huo.

Askofu, ambaye anasaini utangulizi, anakumbuka Petrini wote wanavutiwa na Dunia na maisha yake ya baadaye na kwamba kutokana na kikabiliana kwao ndipo zinajitokeza njia kwa ajili ya ekolojia ili iweze kuachwa kuwa bendera na badala yake iwe ndiyo chaguo.  Hata hivyo mahali pa kuanzia ni mawazo ya Papa Francisko, aliyemshangaza Petrini hasiyesadiki ukweli hadi kuona Papa Francisko anafanya uamuzi wa kwanza wa kwenda Lampedusa, kama ishara ya mshikamano na wahamiaji.

08 September 2020, 13:53