2020.03.19 RADIO VATICAN 2020.03.19 RADIO VATICAN 

Radio Vatican:Kipindi kipya kiitwacho“jina langu siitwi mkimbizi!

Tahere 26 Septemba 2020,Vatican News imezindua kipindi kipya kilichopewa kicha "Jina langu sio mkimbizi”.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

Lengo la kwanza la kipindi cha matangazo ya redio ni dhahiri kutokana na kichwa kisemacho “Mimi jina langu sio mkimbizi”. Njia ya kudhibitisha utambulisho binafsi kinyume na mitindo ya vyombo vya habari ambavyo vinaishia mara nyingi kuelezea hali ya mkimbizi tu kama hali ya kawaida ya tukio la kijamii na kuhusu idadi katika takwimu zilizo baridi kabisa. Mhojiwa, baada ya kutamka jina la programu hiyo, anajitambulisha kwa umma na jina lake, umri, taaluma na asili yake na kila sehemu inaanza hivi na inaisha vivyo hivyo na sauti ya mhusika mkuu ambayo imewekwa ndani ya mada ya programu.

Wimbo pamoja na sauti zake, unataka kukumbusha sifa za kusafiri na umbali na kidokezo cha mashaka, ambayo huandaa kihisia msikilizaji katika mkutano na kile kisichojulikana yaani mawimbi ya bahari yakivunja pwani na filimbi ya kusinyaa na ya kushangaza inatangulia sauti inayotangaza kichwa cha kipinidi hicho; ikifuatiwa na mwendo wa milio ambayo huacha ghafla ili kutoa nafasi kwa mhusika mkuu.

Kiukweli kipindi hiki kinakuja na uhai wake kutoka tayari na sauti ya utangulizi na kila wakati ni sawa swa na inaweza kutambulika kwa urahisi, lakini imebinafsishwa na sauti ya mkimbizi. Usimulizi wa wasifu unachochewa na maswali ya muhoji ambayo karibu hupotea katika awamu ya uhariri. Haya ni mahojiano yaliyofanywa kwa cha za miguu, kwa ujasiri na uelewa; hivi ni viungo viwili msingi vya kufanikiwa kwa programu hii.

Sauti ya muhojiwa pia inaambatana na hadithi hiyo na hatua fupi ambazo huimarisha maelezo na mazingira ambayo nyakati tofauti za hadithi zinawekwa. Knacho boresha vipindi tofauti ni mwingilio wa muziki, iliyochaguliwa kwa msingi wa kijiografia au asili ya kikabila ya mhusika mkuu. Mbali na kila kitu, pia kuna safu milio ya sauti zilizoundwa kuwezesha usikivu wa msikilizaji na utambulisho wake katika matukio yanayosimuliwa. Hivyo hivyo, mabadiliko kwenye jukwa la  Habari ya Vatican na usambazaji kupitia mitandao ya kijamii zinalenga kuhusisha, kuwaarifu, kuwafanya wengine wakutane ambapo  mara nyingi hatuna uwezo wa kufanya hivyo.

26 September 2020, 18:00