Tafuta

2020.09.23 KARDINALI ANGELO SODANO 2020.09.23 KARDINALI ANGELO SODANO 

Matashi mema ya Papa kwa Kardinali Sodano

Ilikuwa ni tarehe 23 Septemba 1950 wakati alipopewa daraja la Upadre na Papa Francisko amependelea kumshukuru kwa huduma yake ya muda mrefu kwa Kanisa na Vatican.

OSSERVATORE ROMANO

Papa Francisko ameelezea "shukrani zake kwa ujumbe kwa Kardinali Angelo Sodano siku ambayo ameadhimisha miaka sabini tangu alipowekwa wakfu wa kikuhani, kwa huduma yake ya uaminifu na bidii ya uongozi wake kwa Kanisa na Vatican. Pamoja na pongezi zake katika maadhimisho, hayo amempatia baraka zake za kitume.

Asubuhi, Jumatano, tarehe 23 Septemba 2020 Kardinali ameadhimisha Misa takatifu katika Kikanisa chake kwa faragha. Baadhi ya washiriki wake walikuwepo. Katika maadhimisho hayo, Kardinali Sodano, awali ya yote amependa kumshukuru Mungu kwa zawadi ya ukuhani wake na kwa utumishi wake wa mrefu kwa Makao makuu Vatican, akimshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa maneno aliyomwambia. Na kwa kumbukumbu yake imemjia ya tarehe hiyo 23 Septemba 1950 wakati alipopokea, pamoja na wenzake  nane katika seminari, wakfu katika Kanisa Kuu la  Asti nchini Italia mikononi mwa askofu wake Umberto Rossi.

Ikumbukwe Kardinali Angelo Sodano, ni Dekano mstaafu wa Baraza la Makardinali aliyezaliwa mwaka 1927. Akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 23 Septemba 1950. Akateuliwa na Mtakatifu Paulo VI kuwa Askofu na kuwekwa wakfu tarehe 15 Januari 1977. Tarehe 30 Novemba 1978 akateuliwa kuwa Askofu mkuu. Ilikuwa ni tarehe 28 Juni 1991 Mtakatifu Yohane Paulo II alipomteuwa kuwa Kardinali.

23 September 2020, 15:43