Tafuta

Vatican News
2019.07.12 Makataba wa Burkina Faso na Vatican. 2019.07.12 Makataba wa Burkina Faso na Vatican. 

Makubaliano juu ya kutambuliwa kwa Kanisa nchini Burkina Faso yameanza kazi yake!

Yameanza rasimi kufanya kazi makubaliano kati ya Vatican na Burkina Faso kuhusu hali ya kisheria ya Kanisa Katoliki katika nchi hiyo ya kiafrika.Mkataba huo ulitiwa sahini kunako tarehe 12 Julai 2019.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 7 Septemba 2020 kupitia taarifa rasimi ya Ubalozi wa Burkina Faso iliyopo makao makuu Vatican, inathibtisha juu ya utaratibu wa kubadilishana Hati za Kurekebisha Mkataba kati ya Vatican na Nchi ya Burkina Faso kuhusu hadhi ya kisheria ya Kanisa Katoliki nchini Burkina Faso, iliyosainiwa huko Vatican mnamo tarehe 12 Julai 2019, leo hii  umekamilika.

Makubaliano ya kuhamasisha na kukuza wema wa wote

Makubaliano yaliyotajwa hapo juu, na ambayo yameanza kutumika kuanzia tarehe 7 Septemba 2020  kulingana na kifungu cha 18, yanahakikishia Kanisa katoliki uwezekano wa kutekeleza kwa dhati utume wake nchini Burkina Faso. Hasa, kwa namna ya pekee kutambuliwa uwepo wake kisheria wa Kanisa na taasisi zake zote. Sehemu zote mbili pamoja na kulindwa uhuru na kujigemea  mamb ambayo ni yao  wenyewe, zijitahidi kushirikiana kwa ajili ya  ustawi wa maadili, kiroho na mali ya mwanadamu na kukuza faida ya pamoja.

Sahini ya makubaliano

Ilikuwa ni tarehe 12 Julai 2019 wakati, katika chumba cha Mikataba mjini Vatican, yalisainiwa makubaliano juu ya hadhi ya kisheria ya Kanisa Katoliki nchini  Burkina Faso na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican kwa ajili ya Mahusiano na ushirikiano wa nchi za Nje  na  kwa upande wa nchi ya Burkina Faso, alikuwa ni Alpha Barry, Waziri wa Mambo ya nchi za nje na Ushirikiano. Kwa kufanya hivyo makubaliano hayo yanahakikishia Kanisa uwezekano wa kutekeleza kikamilifu utume wake nchini Burkina Faso.

07 September 2020, 12:48