Tafuta

Vatican News
Moto kurudia kuunguza bandari ya Beirut nchini Lebanon Moto kurudia kuunguza bandari ya Beirut nchini Lebanon  (ANSA)

Lebanon:ziara ya Katibu Mkuu wa Caritas Internationalis

Kuratibu pamoja na Kanisa mahalia misaada na mipango ya ujenzi na ukarabiti kwa mpya ndiyo moja ya lengo msingi la safari nchini Lebanon ya Aloysius John Katibu Mkuu wa Caritas Internationalis.Mpango wa ziara hiyo ni kukutana na Kardinali Bechara Rai na viongozi wengine.Katika mahojiano na Petrosilli anasema mkutano utakuwa ni kutathimini mahitaji ya watu ili kujikita kwenye matendo yenye ufanisi.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ni zaidi ya mwezi tangu janga la mlipuko mkubwa katika Bandari ya Beirut nchini Lebanon ambao umesababisha zaidi ya vifo vya watu 200, majeruhi 6000 na watu 300,000 kubaki bila makazi. Katika muktadha huo jitihada kwa ajili ya Lebanon kwa njia ya mashirika ya upendo ya Makanisa ulimwenguni bado hayajachoka kuhimiza ili kuweza kukidhi mahitaji ya lazima kwa watu waliopatwa na mkasa huo. Katika nchi hiyo inayojulikana sana kwa utamaduni wake wa udugu na mizizi ya kidini bado wito wa kutiwa moyo na Papa Francisko umesikika, ambao umepelekwa na Katibu wake Kardinali Pietro Parolin hivi karibuni katika ziara yake aliyoitimiza tarehe 4 Septemba 2020, ikiwa ni katika siku hiyo ya  baada ya mwezi mmoja tangu mlipuko huo kutokea. Katika siku huyo ilifanyika hata Siku ya maombi kwa ajili ya ulimwengu wote na kufunga kwa ajili ya nchi ya Lenanon kwa utashi wa Papa Francisko. Kwa wakati huo huo, idadi kubwa ya makanisa ulimwenguni wameweza kuandaa vipindi vingine maalum vya sala na mshikamano vilivyoanzishwa katika mabaraza ya Maaskofu na Caritas Interanationalis imezindua kampeni ya mfuko wa fedha kwa ajili ya Lebanon.

Jumamosi tarehe 12 Septemba 2020 katibu Mkuu wa Caritas internationalis Aloysius John amekwenda nchini Lebanon ili kukutana na viongozi wakuu wa dini na wajumbe wa Caritas mahalia na Ofisi ya  Kanda ya Nchi za Mashariki, kwa lengo la kuratibu vizuri msaada wa binadamu kimataifa na mipango mengine ya ujenzi kwa upya wa nyumba, shule na hospitali vilivyo haribiwa au kupata madhara ya mlipuko. Kwa mujibu wa mhusika kutoka ofisi ya Caritas Bi. Marta Petrosilli ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Caritas Intenationalis amesema,“lengo la safari hiyo ni kuonesha ukaribu wa Caritas intenationalis kwa watu wa Lebanon, lakini kwa ujumla, Katibu Mkuu atakuwa na fursa ya kuhakikisha tathimishi za mahitaji ya watu na msaada unaoendelea kutolewa, ili hatimaye kuwezesha ufanisi zaidi”. Ziara ya kiongozi huyo inatarajiwa kudumu hadi Alhamisi tarehe 17 Septemba 2020.

Katika mkutano na viongozi wakuu wa Kanisa kwa mujibu wa Bi. Petrosilli amesema itakuwa ni muhimu kwa Kanisa mahalia kufanyakazi kwa kushirikiana pamoja yaani caritas ya Lebano iliyoko Beirut ambayo pia imepata madhara ya mlipuko huo japokuwa watu wake wa kujitolewa wameendela kujokita kupelekea msaada wa hali na mali kwa watu. Zaidi ya vijana 800 wako katika kazi kila siku mchana na usiku ili kuhakikisha wanasaidia watu wakiwasambazia karibu milo 10,000 kwa siku na madawa. Kuna hata uhakikisho wa msaada wa kisaikolojia kwa watu. Watu wa kujitolea aidha  wamesaidia watu wengi hata kusafisha barabara na nyumba zao mahali ambapo kumekuwa na uwezekano.

14 September 2020, 12:50