Tafuta

Vatican News
2020.03.27 Kardinali Luis Antonio Tagle 2020.03.27 Kardinali Luis Antonio Tagle  

Kardinali Tagle ameambukizwa na Covid-19

Mmoja wa wasaidizi wa karibu wa Papa Francisko, Rais wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu ambaye yuko Uffilippini ameambukizwa na virusi vya corona .Kwa sasa yuko karantini akiwa na tumaini.Akiwa Roma kabla ya kusafiri vipimo vilionesha hasi mwanzoni mwa wiki hii.

Na Sr. Angela Rwezaula, - Vatican.

Akizungumza na waandishi wa habari Msemaji wa Vyombo vya habari Vatican amethibitisha kuwa Kardinali Luis Antonio Tagle ameambukizwa Covid-19 hasa mara baada ya vipimo kuonesha chanya alipofika Manila nchini Ufillippini. Rais wa Baraza la Kipapa la Unjilishaji wa Watu pia wa Caritas Internationalis hata hivyo haoneshi dalili zozote japokuwa yuko sasa karantini kwa matumaini ya kupona haraka huko Ufilippini mahali alipofika.

Wakati huo huo msemaji huyo amethibitisha kuwa wanaendelea kuhakikisha mahitaji yote na uchunguzi wa lazima hasa kuwatafuta wale ambao alikutana nao siku zilizopita. Tarehe 7 Septemba  2020 kwa mujibu wa Msemaji wa Vyombo vya habari Vataican Dk. Matteo Bruni amesema kuwa Kardinali alikuwa tayari amepima mjini Roma kabla ya kuanza safari na vipimo vilionyesha hasi. Hii ni kesi ya kwanza kwa Rais wa Baraza la Kipapa kupata maambukizi ya covid-19.

11 September 2020, 18:08