“Jihusishe katika mchezo”,mawazo ya Papa Francisko juu ya mchezo!

Leo asubuhi katika uwanja wa Caracalla wamewasilishaji kitabu kipya kilichochapichwa na jumba uchapishaji Vatican.Kinakusanya safu kadhaa za maoni na Papa.Tafakari hizi zilichukuliwa kutoka katika hotuba alizotoa kwa miaka ya hivi karibuni kwa wanariadha mbalimbali.Mabingwa watatu wamesahini utangulizi:Alex Zanardi,Francesco Totti na mwanariadha wa zamani Tegla Loroupe.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mwongozo mmoja  ambao unaonyesha uwezekano wa kuishi  michezo lakini pia hata maisha yenyewe  kwa mujibu wa kocha mkuu akieleza mambo halisi na ambaye ni Papa Francisko. Hii ndiyo maana na  thamani ya kujikita kujihusisha katika mchezo. Kitabu chenye (kurasa 124 - euro 5.00), kilicho chapishwa na Jumba la Uchapishaji la Vatican kwa kushirikiana na chama cha michezo Vatican. Mawazo ya Papa yaliyochukuliwa ni kutoka katika hotuba muhimu kwa wanamichezo na ambapo yeye mwenye alishiriki katika hafla nyingi ambazo zimemwona pamoja na wanariadha wakiwa ni mabingwa wakuu, wanawake na wanaume wenye ulemavu wa mwili au wa akili, lakini pia watoto na vijana kutoka kila sehemu ya hali ya maisha..

Marejeo yote yaliyokusanywa na kuchaguliwa na Lucio Coco na mapendekezo ni kitabu kidogo cha mfukoni ambacho kinaweza kuwafikia wote na ambacho ni msingowa mazoezi ya kiroho na ya kweli na ni kiongozi kwa kweli kwa wale wote wanaotaka kujielekeza katika utafutaji wa sababu halisi za shauku yao na hasa katika michezo. Haya yote yanathibitishwa na mashuhuda watatu ambao wanaonekana katika utangulizi wa Maneno ya Papa, kwa kutiwa sahini na bingwa wa mpria wa miguu Francesco Totti, mwanariadha wa zamani wa marathon kutoka nchini Kenya Tegla Loroupe(kwa sasa ni mhusika wa Timu ya Wakimbizi wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa) na  Alex Zanardi  ambaye alituma mchango wake mapema kidogo kabla ya kupata ajali mbaya sana ambapo hadi leo anapambana kati ya maisha na kifo.

Jihusishe katika mchezo kinajikita ndani ya mpango wa  “We Run Together”, yaani ‘Tunakimbia Pamoja’ uliozinduliwa na Papa Francisko kunako tarehe 20 Mei 2020 na kuikabidhi kwa wanariadha wa Vatican ambao hivi karibuni wamehitimisha mada ya  hisani kimichezo kwa mara nyingine tena wakiwa na lengo la kuchangi kwa uhai wote mapambano dhidi ya Covid-19 na mwaka 2021, ikiwa hali itawezekana ya kiafya kuwezesha kuandaa Mkutano wa Pamoja unakaoleta pamoja Kituo cha Michezo cha Fiamme Gialle huko Castelporziano.

Kitabu ambacho kimewasilishwa  mjini Roma Jumatatu tarehe 7 Septemba 2020 saa 5.30, katika Uwanja wa michezo wa  “Nando Martellini”, kati ya uzuri wa visima vya kuogelea. Kwa ushiriki wa wanariadha wa kike na kiume ambao wametoa hotuba zao ni pamoja na Giovanni Malagò, rais wa Kamati ya Olimpiki kitaifa nchini Italia, Luca Pancalli, Rais wa Kamati ya wanariadha Walemavu ya Italia, Monsinyo Melchor Sánchez de Toca, Katibu msaidizi wa Baraza Kipapa la Utamaduni pamoja na wanariadha kike na kiume walioko mstari wa mbele katika ulimwengu wa michezo. Mratibu wa Mkutano huo alikuwa ni Dk. Alessandro Gisotti, Makamu mwariri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican.

07 September 2020, 14:04