Tafuta

Vatican News
2019.02.27 SR. ALESSANDRA SMERILLI 2019.02.27 SR. ALESSANDRA SMERILLI 

Deni la kiekolojia:makampuni ya kibiashara yajifunze kufanya malipizi!

Kwa mujibu wa mtawa ambaye pia ni mchumi Sr.Alessandra Smerilli,anasema nchi za Kaskazini ulimwenguni na makampuni yao yanapaswa yafanye kama anavyoelekeza Papa,kuhisi wadeni kwa walio maskini zaidi ambao wanawanyonya rasilimali asili zao.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Nia za Papa Francisko kwa mwezi Septemba 2020 ni kwamba Mtandao wa Kanisa ulimwenguni uweze kusali kwa sababu ya  rasilimali za sayari hii. Katika Muktadha wa Kipindi cha Kazi ya Uumbaji  ambacho kimenza tangu tarehe Mosi Septemba na kitandelea hadi tarehe 4 Oktoba na katika mantiki ya mwaka wa 5 tangu kutangazwa kwa Waraka wa Laudato Si,  Papa Francisko anaelezea wasi wasi wake wa madeni ya kiekolojia, ambayo yanasababisha madhara na unyonyaji wa rasilimali asili, kwa maana hiyo anatoa wito wa kushirikishana kwa namna ya haki na heshima. Sr. Alessandra Smerilli, Mratibu wa 'Tume ya nguvu Kazi ya Uchumi ya Vatican ya  Covid -19' na Profesa wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Sayansi ya Elimu cha Wasalesiani Roma, amehojiwa na Vatican News kuhusiana na mtazamo wake. Akianza kuelezea juu ya tafakari ya mwezi huu anasema kuwa Papa katika sala yake kwa ajili ya  ulimwengu, hasa katika ombi lake la sala, anasema ikiwa rasilimali za sayari zitaporwa, kwanza kabisa, ni wazi, kuwapo uharibifu wa mazingira. Lakini kwa kuwa wale walio matajiri wa rasilimali hizi wako hasa katika nchi zote zenye dharura, nchi ambazo zinazoitwa za Kusini na ambazo zinaibiwa utajiri wao wa asili, hii yote pia inageuka kuwa shida ya kiuchumi. Wakati rasilimali, pamoja na kuwa maliasili, pia ni malighafi ya chakula, kwa njia hiyo pia sisi sote tuna shida kubwa ya usambazaji wa chakula, tuna watu wanaokufa kwa njaa.

Sr. Alessandra aidha amesema katika pendekezo la maombi, ya Papa Francisko pia anatumia picha iliyo rahisi  sana kuthibitisha kuwa tunakamua bidhaa za sayari hiyo kana kwamba ni machungwa. Yeye anataka kusisitiza kwamba tuna tabia isiyo ya heshima kwa wale ambao wana rasilimali hizo. Anazungumza juu ya uporaji kwa sababu ndivyo inavyotokea vitani wakati washindi wanaposhinda nchi na kuchukua utajiri wake wote kama kichaa, wakiacha maafa makubwa nyuma yake. Kwa bahati mbaya hiki ndicho kinachotokea katika maeneo mengi wakati maliasili inapoporwa na katika muktadha huu Papa anaanzisha wazo la deni ambalo linaonekana  kuwa lenye maana.

Papa Francisko anazungumzia juu ya nchi na makampuni ya kibiashara ya Kaskazini yaliyo jitajirisha kwa kunyonya zawadi za asili za nchi za Kusini na kusababisha deni la kiekolojia na anauliza ni nani analipa, kwa njia hiyo , Sr Alessandra anafafanua kwamba ni usemi ambao Papa alikuwa ameuanzisha katika kifungu namba 51  cha Laudato si ', ambapo alifanya ulinganisho unaofaa sana. Kupora, kuraua, kunyonya nchi nyingine kunamaanisha kujitajirisha nyuma yao, kwa maana hiyo ni karibu na kusema kuchukua mkopo wa  rasilimali hizi na kusababisha deni. Na wakati katika uchumi unapokumbana na  deni baadaye ni kuhisi  ulazima wa  kulilipa na kumbe linapokuja suala la ikolojia hatuzingatii. Katika Waraka wa Papa Francisko wa Laudato si unatukumbusha kuwa nchi za Kusini mwa ulimwengu zina deni kwa zile nchi tajiri zaidi. Kuna mipango ya kuingilia katika madeni haya ya kiuchumi ambayo yanawekewa masharti. Hata hivyo kwa unyenyekevu na akili ya Papa  Francisko anajiuliza kwanini hii haifanyiki pia ikiwa ni deni la kiikolojia. Anajiuliza kwanini haturuhusu wale wanaotumia rasilimali za wengine kulipa deni hili  kwa nchi hizo, amefafanua mtawa huyo.

Yeye kama mwanauchumi, jambo linalomgusa sana kuhusu mawazo haya  ya Papa anaamini kwamba lazima kuacha mara moja, leo hii  na siyo kesho, kama asemavyo Papa ya kufikiria uharibifu wa mazingira kama kitu cha nje kwa shughuli za biashara. Kiukweli anasisitiza yanaitwa mambo ya nje, kana kwamba ni athari isiyotarajiwa, hasa ya nje. Hoja ni mjasiriamali lazima azalishe, ili kuzalisha anahitaji rasilimali kadhaa, ananyonya nchi nyingine, anazalisha matatizo ya kiekolojia, lakini haya ni mambayo yanayotokea zaidi ya nia yake.  Lazima tuache kufikira  haya kama kitu cha njebadala yake  lazima tujifunze kuwa haya yote ni sehemu ya shughuli za kampuni na hii lazima ijumuishe shughuli zote zinazohitajika kupunguza athari hii ya kiekolojia kwa gharama zake.

05 September 2020, 16:41