Maandamano nchini Zimbabwe Maandamano nchini Zimbabwe 

Zimbabwe:mshikamano wa Balozi wa Kitume kwa maaskofu

Mwakilishi wa Kipapa katika maeneo ya kiafrika amepeleka mshikamano wake kwa Askofu Mkuu wa Harare mara baada ya shambulio la maneno makali lililofanywa dhidi yake na serikali kufuatia na maaskofu kukosoa usimamizi wa maandamano na matatizo ya kiafya yanayoendelea nchini humo.

Sr. Angela Rwezaula & Fr. Paul Samasumo -Vatican

Serikali ya Rais Mnangagwa haipokei kabisa kuhusu taarifa ya maaskofu wa Zimbabwe iliyomo katika barua ya kichungaji iliyotolewa siku ya  Ijumaa iliyopita kuhusu mwenendo wa taasisi hiyo wakati wa maandamano ya kitaifa na ukandamizwaji uliofuatia mnamo Julai 31 iliyopita. Waziri wa Habari, Utangazaji na Huduma za Redio na Televisheni wa Zimbabwe, Monica Mutsvangwa alitoa taarifa iliyotolewa  tena na televisheni ya kitaifa siku ya Jumamosi jioni, ambapo alishambulia kwa sauti kali  za kuzidisha na kukera hasa  mtu  kama Askofu mkuu Robert Christopher Ndlovu wa Harare,  na ambaye ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Zimbabwe. Na kwa njia hiyo  Balozi wa wa Kitume nchini Zimbabwe Askofu Mkuu Paolo Rudell amekwendaa moja kwa moja kwa moja kwake siku ya Jumapili asubuhi kama kitendo cha ishara ya mshikamano na maaskofu wote wa nchi.

Mgogoro wa kiuchumi na kiafya

Undeshaji mbaya katika  mgogoro wa kiuchumi na kiafya kwa upande wa  serikali ya Emmerson Mnangagwa ulisababisha maandamano makubwa katika mitaa na baadaye kwenye vyombo vya habari vya kijamii, kwa  kampeni yao iitwayo “ #ZimbabweanLivesMatter”. Haya ni maandamano ya watu  ambayo kwa mujibu wa maaskofu wanasema serikali ilijibu kinyume na ambayo imefanya kunyamazisha kila aina zote za ubishani. Hata hivyo Serikali imekosolewa sana kuwa na ukiukwaji wa haki za binadamu ambao umeona polisi na wanajeshi wakitenda dhidi ya wanaharakati, waandishi wa habari na umma. Wachunguzi kadhaa, kama vile Amnesty International, wanaelezea hali ile ya sasa ni kama hali ya woga na ukandamizwaji kikatili, kutoweka, kukamatwa, utekaji nyara wa mitaani na kuteswa kwa sauti kali.

Upo upotoshaji wa taarifa ya kweli kwa raia

Uchunguzi wa maaskofu katika Barua ya kichungaji,na  ambayo katika  taarifa za Waziri Mutsvangwa, hata hivyo ameepuka kujibu, na kwa kwa njia nyingi umepanuliwa na  mawakili wa nchi, wafanyakazi wa kimatibabu na wanaharakati wa nchi. Zaidi ya hayo, waangalizi nchini Zimbabwe walibaini kuwa taarifa ya serikali ilitafuta kupotosha raia katika kupingana na kitendo cha Kanisa Katoliki na matakwa na nafasi za Papa Francisko.

Katika barua ya Maaskofu

“Hofu inazungukia mfupa wa mgongo wa watu wetu wengi leo. Ukandamizaji wa kupingana haujawahi kutokea. Hii ndio Zimbabwe tunayotaka? Kuwa na maoni tofauti - maaskofu wa Zimbabwe wanaandika - haimaanishi kuwa adui. Ni dhahiri kwamba kutokana na tofauti ya maoni, mwanga huzaliwa”. Maaskofu wanaongezea: “Wito kwa waandamanaji ni ishara ya kufadhaika kutokanna na kuongezeka kwa fedheha kwa sababu ya hali ambayo raia wengi wa Zimbabwe hujikuta nayo. Ukandamizaji wa hasira za watu hauwezi kusaidii kitu zaidi ya kuongezea mgogoro na kupelekea taifa katika mgogoro wa kina zaidi”.

Kuhusu uongozi wa kisiasa, maaskofu pia wanasisitiza juu ya kutofaulu kuchukua jukumu la shida za kitaifa, ambazo  zinaweka lawama kwa kile kinachotokea kwa “wageni, ukoloni, na kwa kile kijulikanacho  kama wadadisi wa ndani”. Kutokana na hilo maaskofu wanauliza swali: “Ni lini tutachukua majukumu yetu? Wakati majirani zetu katika kanda, maaskofu wanaandika  wako wanaimarisha taasisi zao za kidemokrasia na sisi utafikiri tunaonekana kuwa tunadhoofisha majukumu yetu”. Hata hivyo kuonesha kukata tamaa kwa maneno ya maaskofu pia ni kutokana na  ukosefu wa nafasi ya upatanisho uliyotolewa na Afrika Kusini pia kwa usambazaji usio sawa wa zana za kiafya muhimu ili kukabiliana na janga la Covid-19”.

Wito kwa ajili ya amani na ujenzi wa kitaifa

Barua ya maaskofu katoliki nchini Zimbabwe inafunga kwa kutoa wito wa haraka ambao unaongezea ujumuishaji, mazungumzo na uwajibikaji: “Tunatoa wito wa  haraka  kwa ajili ya  amani na ujenzi wa kitaifa kupitia jitihada, majadiliano na jukumu la pamoja kwa ajili ya mabadiliko. Tunajua pia kuwa janga la Covid-19 litatuelekeza kwenye changamoto mpya kwa siku sijazo. Kiukweli, kama John Lewis alivyoelewa, kwamba kamwe maandamano hayamaliziki, lakini kwa pamoja tutayashinda”.

Wakatoliki na wasio Wakatoliki kuwa upande wa Maaskofu

Kwa upande wao, Wakatoliki na wasio Wakatoliki nchini Zimbabwe wameonesha mshikamano wao kwa maaskofu kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Kwa namna ya pekee, wamekumbusha mawaziri, wahudumu na maafisa kwamba maaskofu ni wachungaji ambao hawana nia ya kuingilia siasa lakini ambao hawawezi kukaa kimya mbele ya mateso mengi ya kijamii na umaskini mwingi.

17 August 2020, 14:06