Tafuta

Vatican News
Uwanja wa Mtakatifu  Damaso Vatican Uwanja wa Mtakatifu Damaso Vatican  

Vatican:tarehe 2 Septemba kuanza kwa upya ushiriki wa waamini katika katekesi za Papa!

Kuanzia Jumatano tarehe 2 Septemba 2020 ushiriki wa waamini kwa mara nyingine tena wa Katekesi ya Papa Fracìncisko utaanza lakini kwa kufuata kanuni za kiafya.Waamini wanaopenda wataunganika katika uwanja wa Mtakatifu Damaso,kiingilio ni bure bila kuwa na tiketi.Njia ya kuingilia ni kupitia upande wa kulia wa uwanja wa Mtakatifu Petro.

VATICAN NEWS

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa vyombo vya habari Vatican wamethibitisha kuwa Katekesi ya Papa ndani ya Maktaba ya Jumba la kitume haitafanyika tena, na badala yake itaanza kwa upya kwa ushiriki wa waamini kwa kufuata kanuni za kiafya.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msemaji huyo ni kwamba kuanzia mwezi ujao, Jumatano tarehe 2 Septemba 2020  kwa hakika katekesi ya Papa itaweza kuwa na ushiriki wa waamini wote wanaopenda.

Kuingia ni bure kuanzia saa 1.30 asubuhi.

katika taarifa hiyo “Kwa kufuata maelekezo ya kiafya kutoka kwa mamlaka, katekesi ya Papa itafanyika katika uwanja wa Mtakatifu Damaso kuanzia saa 3.30, majira ya asubuhi. Washiriki wote ambao wanapenda kuudhuria hawana haja ya tiketi ya kuingilia; na lango iltafunguliwa kuanzia saa 1:30 asubuhi  kupitia upande wa kulia wa uwanja wa Mtakatifu Petro”.

26 August 2020, 13:48