Tafuta

Vatican News
2020.06.16 silaha za kinyuklia, Asia 2020.06.16 silaha za kinyuklia, Asia  

Vatican inaunga mkono jitihada za UN kupiga marufuku majaribio ya silaha za kinyulia!

Vatican iko tayari kabisa kuunga jitihada za Umoja wa Mataifa ili kufikia kuweka mkataba wa kupiga maruku kwa ujumla wa kufanya mazoezi ya silaha za kinyuklia (CTBT),uliowekwa kunako mwaka 1996.Hayo yamesema katika mkutano wakati wa kuelekea kwenye kilele cha Siku ya Kimataifa ya kudhibiti mjaribio ya silaha za kinyuklia kila ifikapo tarehe 29 Agosti ya kila mwaka.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Vatican iko tayari kuunga mkono juhudi za UN katika kuingia  kufanya Mkataba wa kupiga marufuku kwa ujumla ya kufanya majaribio  ya nyuklia (CTBT), uliosainiwa mnamo 1996. Amesema hayo Monsinyo Frederik Hansen mwakilishi katika Utume wa kudumu wa Vatican kwenye Ofisi ya  Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, jijini New York,  Marekani, tarehe  26 Agosti 2020 katika fursa ya Mkutano kwa njia ya mtandao wa  kukumbuka na kuhamasaisha “Siku ya Kimataifa ya kudhibiti majaribio ya Kinyuklia”,  ifanyikayo kila tarehe 29 Agosti. Imepita robo tatu ya karne tangu walipofanya majaribio ya kwanza  ya silaha za kinyuklia, ijukanayo  “trinity ,katika majaribio yaliyofanyika kwenye  jangwa la Mexico mpya  huko Marekani”. Na tangu wakati huo wameweza kufanyia  katika eneo hilo mazoezi zaidi ya 2000 na miongoni mwake, saba ni katika karne hii na kusababisha madhara makubwa ya mazingira na madhara ya afya za watu wanaoishi katika maeneo hayo walimo fanyia majaribio au kuelekea mahali pengine kwa njia ya upepo kwenye mionzi iliyoachwa katika anga. Ni matumaini ya kwamba majaribio yaliyofanywa miaka 3 ya mwisho yawe ndiyo mwisho kabisa wa matuko hayo kwa mujibu wa Monsinyo Hansen.

Tume ya mkataba wa kupiga marufuku inafanya kazi na mataifa 8

Kwa sababu hii ni muhimu kwamba Tume ya Maandalizi ya Mkataba huo wa kupiga marufuku ya mazoezi  ya kinyuklia inafanya kazi pamoja na Mataifa nane makuu ambayo kwa  kuridhia kwao ni muhimu ili kuweza kuingia kwa makubaliano hayo ya mkataba amefafanua  Monsinyo Hansen na kwamba Mataifa haya yanaamini  kuwa usalama wa kitaifa na kimataifa utaimarishwa tu ikiwa  mkataba huu (CTBT) utaweza kuingia kafanya kazi. Majaribio ya nyuklia, kiukweli, yatapunguza ukosefu wa salama wa ulimwengu na  kwa maana hiyo kuwa na amani na utulivu wa wanachama wote wa UN na watu wanaowawakilisha. Mkataba huo, kwa njia hiyo  amesisitiza ni hatua msingi ya ya kuunda ulimwengu usio kuwa na silaha za nyuklia.

Ni miaka 75 tangu kulipuka kwa bomu la atomiki huko Hiroshima

Katika mwaka ambao  unaadhimisho miaka 75 tangu kulipuka  bomu la atomiki, kwa kukumbuka waathiriwa, Monsinyo  Hansen amewaalika viongozi wote kurudia tena kuwa na roho ambayo ilianzishwa na Umoja wa Mataifa na kuwafikia wote kwa pamoja  na si tu ulazima wa kudumu, lakini kutofanya majaribio  kabisa ya silaha za nyuklia,na hili ndilo lengo la ulimwengu bila kuwa na  silaha za nyuklia  na kwamba  lengo hili pia limeoneshwa zaidi katika muktadha wa janga la ulimwengu ambalo limeonyesha zaidi upuuzi wa kutumia rasilimali muhimu katika utunzaji wa silaha za maangamizi wakati katika  sayari ya dunia watu wengi wanapambana namna ya kuweza kuishi.

Maneno ya Papa Francisko  Hiroshima

Akitaja maneno ya Papa Francisko aliyotamka wakati wa kutembelea Hiroshoma akiwa katika ziara yake ya kitume mwezi Novemba mwaka jana Monsinyo Hansen amesema “matumizi ya nishati ya atomiki kwa madhumuni ya vita leo hii  ni zaidi ya uhalifu  na sio tu dhidi ya hadhi ya wanadamu, lakini pia dhidi ya mustakabali ujao na unaofaa katika nyumba yetu ya pamoja na kwamba pia matumizi ya nishati ya atomiki kwa madhumuni ya vita ni tabia mbaya kimaadil, kama vile ilivyo mbaya kimaadili kumilki  silaha za nyuklia.

27 August 2020, 14:16