Tafuta

Vatican News
Siku ya Kimisionari ulimwengu mwaka 2020 itafanyika tarehe 18 Oktoba bila mabadiliko yoyote. Siku ya Kimisionari ulimwengu mwaka 2020 itafanyika tarehe 18 Oktoba bila mabadiliko yoyote. 

Maadhimisho ya Siku ya Kimisionari ulimwenguni ni tarehe 18 Oktoba 2020!

Katika taarifa iliyotolewa na Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu,linathibitisha kuwa Siku ya Kimisionari mwaka huu kwa ngazi ya ulimwengu itafanyika siku ya Dominika tarehe 18 Oktoba bila mabadiliko yoyote yale katika kalenda.

Katika kujibu baadhi maswali waliyoomba kujua juu ya maadhimisho ya Siku ya Kimisionari ulimwenguni kwa  2020, kwa mujibu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu, wanathibitisha kuwa maadhimisho hayo mwaka huu kwa ngazi ya ulimwengu, itafanyika  siku ya Dominika tarehe 18 Oktoba, bila kuwa na mabadiliko yoyote katika kalenda. Kwa mujibu taarifa iliyotolewa  aidha wanabainisha kuwa tayari majimbo mengi yamekwisha anza kwa muda maandalizi lakini bado inabaki uhamasishaji wa kimisionari kwa upande wa watu wa Mungu.

Imani ya kimisionari

Katika kuhitimisha taarifa yao wanasema imani, kiukweli, asili yake ni ya umisionari na maadhimisho ya Siku ya Kimisionari ulimwenguni kusaidia kubaki na mwelekeo huo muhimu wa imani ya Kikristo iliyo hai kwa waamini wote.  Baraza la kipapa la Unjilishaji wa Watu aidha linakumbusha maana ya ushirikiano na uwajibikaji wa maaskofu na kusisitiza kwamba ukusanyaji wa sadaka kwa Siku hiyo ni kwa ajili ya Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari,ambayo hufanya kazi katika muktadha huo wote  wa ulimwengu kwa msaada ulio sawa wa Makanisa katika maeneo ya kimisionari.

28 August 2020, 15:44