Tafuta

Vatican News
2020.08.28 Papa Francisko atembelea Kaburiri la Mtakatifu Monika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Agostino huko Campo Marzio Roma 2020.08.28 Papa Francisko atembelea Kaburiri la Mtakatifu Monika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Agostino huko Campo Marzio Roma 

Papa Francisko atembelea Kanisa la Mtakatifu Agostino-Campo Marzio,Roma

Tarehe 27 Agosti mchana katika siku ya kukumbuka Mtakatifu Monika,Papa Francisko amekwenda kutembelea Kaburi la Mtakatifu monika linalohifadhiwa ndani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Agostino huko Campo Marzo,Roma linalo mahali ambapo amejikita kwa sala ya kimya katika Kikanisa kidogo hicho.

VATICAN NEWS

Katika siku ambamo mama Kanisa anakumbuka Mtakatifu Monika, mama yake Mtakatifu Agostino, Papa Francisko tarehe 27 Agosti 2020 amekwenda katika Kanisa Kuu ambalo linatunza kaburi la Mama wa Mtakatifu Agostino kusali.

Kwa mujibu wa msemaji wa vyombo vya habari Vatican "Papa Francisko amekwenda katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Agostino huko Campo Marzio, Roma ambapo amejikita kwa sala ya kimya katika Kikanisa kidogo cha Mtakatifu Monika mahali ambao kuna kaburi na baada ya sala amerudi mjini Vatican".

28 August 2020, 13:48