VATICAN-DINI - PAPA VATICAN-DINI - PAPA  

Mshikamano wa kidini unahitajika katika huduma ndani ya dunia iliyojeruhiwa na Covid-19!

Jibu la kiekumeni na kidini kwa wakati huu na mshikamano kwa ajili ya kukabiliana na wakati ujao wa ulimwengu unaokatizwa na janga,ndiyo kiini cha hati ya pamoja ya tafakari na ya kutia moyo iliyoandikwa kwa pamoja na Baraza la makanisa Ulimwenguni(WCC)na Baraza la Kipapa la majadialiano ya kidini (PCID).

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kuhamasisha Makanisa na mashirika ya kikristo ili kutafakari umuhimu wa mshikamano wa kidini kwa namna ambavyo ulimwengu umejeruhiwa na janga, ndiyo lengo la hati ya pamoja iliyoandikwa na Baraza la Makanisa Ulimwenguni (WCC) na la Kipapa la Majadiliano ya kidini (PCID) kwa kuupatia jina “kuhudumia dunia iliyojeruhiwa katika mshikamano wa kidini. Ni mwaliko wa kikristo katika kutafakari na matendo ya dhati katika wakati wa COVID-19”. Kwa mujibu wa hati hiyo ya pamoja wamefikiria hata kwa maana ya kuwasilisha katika dini zote ambazo zimetoa majibu ya Covid-19 kwa mawazo yanayofanana ambayo ni msingi wa tamaduni binafsi.

Mshikamano unasaidiwa na tumaini

Katika taarifa iliyotolewa uhusu hati yao ya pamoja ni kwamba wanatambua mantiki ya sasa ya janga kama kipindi cha kugundua mitindo mbali mbali ya mshikamano kwa ajili ya kufikia mstakhabali wa kesho. Hati hiyo imeunda na vipengele vitano, baada ya utangulizi, hati hiyo inatafakari maumbile ya mshikamo inaosaidiwa na tumaini na kutoa msingi wa kikristo wa mshikamano wa kidini na kwa maana hiyo unaonesha ufunguo na kuorodhesha mambo kadhaa yanayotakia  kufuata kama vile tafakari juu ya mshikamano ambao unaweza kutafisriwa kama matendo ya dhati na yanaoyoaminika.

Janga kufunua madhaifu ya binadamu

Kardinali Miguel Ángel Ayuso Guixot, Rais wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini, amebanisha kuwa huduma ya kikristo na mshikamano katika dunia iliyojeruhiwa, viko katika ratiba ya kila siku kwenye shughuli  za taaisis hizo mbili tangu mwaka jana. Janga limesukuma mpango huo kutendwa kama kutoa  jibu la kiekumene na kidini kwa wakati na ambapo pia janga limeweka mwanga zaidi wa majeraha na udhaifu wa ulimwengu wetu, huku ukionesha kuwa majibu yetu, lazima yatolewe kwa njia ya mshikamano wa pamoja, uliowazi kwa wafuasi wa tamaduni tatu za kidini na watu wote wenye mapenzi mema, kwa kufikirai wasiwasi kwa ajili ya ubinadamu wote.

Familia ya kibinadamu kukabiliana na kulinda mwingine

Naye Katibu Mkuu wa mpito wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni WCC, profesa Ioan Sauca, amebainisha kuwa mazungumzo ya kidini ni maisha kwa ajili ya kuponyesha na utunzaji wa mmoja na mwingine kwa ngazi ya ulimwengu. Mbele ya janga hili familia ya kibinadamu iko inakabiliana kwa pamoja na wito usiokatika wa kulinda mmoja na mwingine na zaidi kuokoa jumuia zetu. Majadiliano ya kidini yanasaidia si tu kuweka wazi misingi ya imani yetu na utambulisho wetu kikristo lakini pia utambulisho na uelewa wetu wa changamoto na suluhisho bunifu ambazo wengine wanaweza kuzitoa.Hati hiyo ndiyo ya mwisho kutengenezwa na WCC na Baraza la Kipapa la majadiliano ya kidini mara baada ya kuchapishwa kwa  ile ya “Elimu ya Amani katika Ulimwengu  wa dini nyingi”,  mtazamo mmoja wa Kikristo ya mwezi Mei 2019.

27 August 2020, 16:04