Tafuta

Vatican News
Ni mtu, Jumuiya na watu ambao wanapaswa wawe kitovu na waliounganishwa kwa ajili ya kuponya, kwa ajili ya kutunza na kwa ajili ya kushirikishana Ni mtu, Jumuiya na watu ambao wanapaswa wawe kitovu na waliounganishwa kwa ajili ya kuponya, kwa ajili ya kutunza na kwa ajili ya kushirikishana 

Kard.Parolin:Kipaumbele cha maisha sio uchumi ni binadamu!

Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican katika mahojiano na Carlo Di Cicco yaliyotangazwa Alhamisi tarehe 27 Agosti katika Tovuti ya www.ripartelitalia.it anasema kipaumbele cha maisha siyo uchumi bali ni mwanadamu.Anakumbusha maneno ya Papa:"Ni mtu, Jumuiya na watu ambao wanapaswa wawe kitovu na waliounganishwa kwa ajili ya kuponya,kutunza na kwa ajili ya kushirikishana.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

Janga linaendelea kutufundisha namna ya mgogoro ambao hakuna anayeweza kuondokana nao peke yake. Ili kuweza kukabiliana na virusi kuna haja ya kutoa jibu shirikishi na uratibu. Hayo pia yanafaa katika kuponyeshwa na mabaya ya kutojali, upweke na uadui. Ndiyo uthibitisho la Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican katika mahojiano na Carlo Di Cicco yaliyotangazwa Alhamisi tarehe 27 Agosti katika Tovuti ya www.ripartelitalia.it. Pamoja na hayo yote kipaumbele siyo uchumi anaeleza Kardinali. Covid-19 haikusababisha mgogoro wa kiafya tu bali pia iimeleta pigo katika mantiki nyingi za maisha ya mwanadamu, kuanzia familia, kisiasa, kazi, makambuni, biashara, utalii na mengine mengi. Tabia iliyotanda na kusukana kwa janga la virusi, inaturudisha kukumbusha maneno ya Papa Papa Francisko kwamba kila kitu kimeunganika kati yake.

Kwa mujibu wa Katibu wa Vatican, anasema ikiwa serikali zimelazimisha kuchukua hatua kali hadi kufikia kusimamisha shughuli za kiuchumi ili kupambana na janga, ina maana kipaumbele siyo uchumi bali ni mwanadamu. Hii ina maana awali ya yote kutunza afya. Pamoja na hayo Mafundisho jamii ya Kanisa, ambayo yametanda mzizi wake katika elimu ya mtu mkristo, inatukumbusha kuwa haiwezekani kuzuia kutunza afya ya mwili tu. Inatakiwa kufungamanisha kutoka kwa mwanadamu ambaye anapaswa kwa njia hiyo kuwa lengo msingi la jitihadaza za kisiasa na kiuchumi katika maadili ya uwajibikaji shirikishi katika nyumba yetu ya pamoja. Matokeo yake,  hayo Kanisa linaalikwa kuwa na  wito wa uchumi katika huduma ya mtu, ili kuhakikisha kila mwanadamu anakuwa katika hali yake ya lazima kupata maendeleo ya kibindamu fungamani na maisha yenye hadhi.  Leo hii kuliko awali alisema Papa Francisko wakati wa Siku Kuu ya Pasaka tarehe 11 Aprili iliyopita kwamba “Ni mtu, Jumuiya na watu ambao wanapaswa wawe kitovu na waliounganishwa kwa ajili ya kuponya, kwa ajili ya kutunza na kwa ajili ya kushirikishana”.

Kwa mujibu wa Kardinali Parolin, anasema hatari nyingine ambazo zimejitokeza katika mapambano dhidi ya janga hilo kwa maana nyingine  ni lazima zikumbukwe, kama vile kuongezeka kwa njia za kupunguza maoni ambayo, kwa kuzingatia afya ya mwili, uhatarisha kuzingatia  tu viwango vya kiroho visivyofaa. Katika hali ya dharura kubwa kama hi ambayo tumezingirwa  na kufanana kama isiyo na  kikomo cha tafsiri ya masuala  ya kiafya kulingana na dhana za kiufundi na ambayo, imekataa mahitaji kadhaa  msingi, kwa mfano kwa kuzuia ukaribu wa wanafamilia na msaada wa kiroho kwa wagonjwa na wanaokaribia kufa. Hii inahitaji kwamba tuendeleze kutafakari kwa kina juu ya maswali mengi ambayo janga hili limeweka mbele yetu, Kardinali amesisitiza. Hata hivyo ameongeza kusema janga hilo limefunua kutegemeana kwetu na udhaifu wetu  na udhaifu unaotuunganisha pamoja. “Wakati mantiki ya kuzuia nyuklia ilitawala, Mtakatifu Yohane  XXIII, katika waraka wake wa Pacem in terris, alisisitizia juu ya kutegemeana kati ya jamuiya  za kisiasa kwamba“ Hakuna jumuiya ya kisiasa leo inaweza kufuata masilahi yake na kuendeleza kwa kujifungia yenyewe binafsi”, amkumbusha Kardinali.  Na Baba Mtakatifu Francisko katika maandishi yake kwenye Waraka wa  Laudato  si anasisitiza kuwa  “Utegemezi unatulazimisha kufikiria ulimwengu mmoja, na  mpango wa pamoja”. Kwa upande mwingine Mtakatifu Yohane Paulo II  alikumbuka katika  waraka wake wa ‘Sollicitudo rei socialis’  kwamba  “leo hii  tunakabiliwa na kutegemeana kiteknolojia, kijamii na kisiasa, ambavyo vinahitaji haraka maadili ya mshikamano”.

Pamoja na hayo yote leo hii, badala ya kupendelea ushirikiano kwa ajili ya  faida ya wote ulimwenguni, Kardinali anasema tunaona kuta zaidi na zaidi zikijengwa karibu nasi, zinavuka  mipaka kama dhamana ya usalama na kufanya kuendesha mfumo wa ukiukwakaji wa sheria, kwa  kudumisha hali ya mizozo ya kudumu ya ulimwengu”. Kama vile Baba Mtakatifu Francisko alivyokumbuka huko Nagasaki, kuwa  “matumizi ya silaha yalifikia kilele chake mnamo 2019, na sasa kuna hatari kubwa kwamba, baada ya kipindi cha kupungua, pia kwa sababu ya vizuizi vinavyohusishwa na janga hili, inaendelea kuongezeka”. Kwa maana hiyo wakati huu inaonyesha, badala yake, kwamba lazima tupande urafiki na wema kuliko chuki na woga. Kwa kuongezea, amesema kutegemeana kwa sayari kunahitaji majibu ya ulimwengu katika shida za hapa na pale. Papa Francisko alisisitiza  piakatika mkutano wake na Wamaharakati maarufu mwaka 2015   kuwa “kwa sababu ya utandawazi wa matumaini [...] lazima ubadilishe utandawazi huu wa kutengwa na kutojali”!

Katika suala hili, Kardinali  Parolin amesema kuwa  “mfumo wa kumbukumbu uliochorwa picha na Baba Mtakatifu Francisko kwa ajili ya  uchumi unapatikana zaidi ya yote katika Waraka wa  ‘Laudato si’ , ambao pia unakuza kwa dhati ule wa  ‘Caritas’wa Papa Mstaafu  Benedikto XVI. Hizo ni ‘ensaiklopidia’ mbili kubwa za hivi karibuni za kijamii. Papa Mstaafu Benedikto XVI alizungumzia uchumi ambao unapaswa upate nafasi ya mantiki  ya zawadi,  msingi wa kutoa bure ambao unajifafanua tu kwa njia ya mshikamano, lakini hata undani zaidi  wa udugu wa kibinadamu. Papa Francisko alizindua kwa mara nyingine tena mada msingi ya maendeleo fungamani ya kibinadamu katika muktadha wa kiekolojia fungamani, mazingira, uchumi, kijamii, kitamaduni, na kiroho. Mafundisho kijamii ya Kanisa, ambayo wengi wanatambua uthabiti msingi na mwelekeo, unaonyesha  kujua jinsi ya kusasisha kila wakati ili kujibu maswali ya ubinadamu kwa usahihi, mshikamano na maono ya jumla .

Leo hii janga hili linaleta mshtuko mkubwa katika mfumo mzima wa uchumi na kijamii na ukweli wake unafikiriwa, katika ngazi zote, Kardinali Parolin amethibitisha. “Shida za ukosefu wa ajira, anashutumu, ni kubwa na zitakuwa kubwa, shida za afya ya umma zinahitaji mapinduzi ya mifumo mzima ya afya na elimu, na jukumu la serikali na uhusiano kati ya mataifa hubadilika. Kanisa linahisi kuitwa kusindikiza njia ngumu iliyo mbele yetu sisi wote kama familia ya wanadamu. Na lazima ifanye kwa unyenyekevu na busara, lakini pia na ubunifu. Kwa upande wa Kardinali Parolin, kwa kifupi, anabainisha kwamba kuna kanuni thabiti za kurejea, lakini leo hii ubunifu wa ujasiri ni wa haraka sana kuliko hapo awali kwa sababu mgogoro mkubwa wa janga hili usiishie katika msiba mbaya sana badala yake uweze kufungua nafasi za uongofu wa kibinadamu na kiikolojia ambao ubinadamu unahitajika.  Kwa kuhitimisha, katibu wa Vatican anatumaini kwamba yale yote yaliyofanyiwa uzoefu katika miezi ya kwanza ya janga yameimarisha kwa waamini wengi ufahamu mkubwa wa maisha ya sakramenti, pamoja na shauku na matarajio ya ushiriki hai mzuri zaidi katika liturujia ambayo ni kilele na chanzo cha maishayote ya Kanisa.

29 August 2020, 16:01