Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Juvita Rodrigues De Ataide Goncalves kutoka Timor ya Mashariki Baba Mtakatifu Francisko amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Juvita Rodrigues De Ataide Goncalves kutoka Timor ya Mashariki 

Balozi wa Timor ya Mashariki Awasilisha Hati za Utambulisho kwa Papa Francisko!

Balozi Juvita Rodrigues Barreto De Ataíde Gonçalves alizaliwa kunako tarehe 30 Juni 1973 huko Tiba, Timor ya Mashariki. Ameolewa na kubahatika kupata watoto watano. Kitaaluma ni mhasibu aliyejipatia shahada yake ya uzamivu kutoka katika katika Chuo Kikuu cha “East Timor Institute of Business”. Balozi Juvita ni mbobezi katika masuala ya fedha na ujasiriamali kwa wanawake.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 28 Agosti 2020 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Bi Juvita Rodrigues Barreto De Ataíde Gonçalves, Balozi mpyaTimor ya Mashariki mjini Vatican. Balozi Juvita Rodrigues Barreto De Ataíde Gonçalves alizaliwa kunako tarehe 30 Juni 1973 huko Tiba, Timor ya Mashariki. Ameolewa na kubahatika kupata watoto watano. Kitaaluma ni mhasibu aliyejipatia shahada yake ya uzamivu kutoka katika katika Chuo Kikuu cha “East Timor Institute of Business”.

Katika maisha yake, Bi Juvita Rodrigues Barreto De Ataíde Gonçalves,  amewahi kufanya kazi katika taasisi na makampuni mbali mbali ya fedha kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2010. Baadaye kati ya mwaka 2012 hadi mwaka 2016 akateuliwa kuwa mkurugenzi na mshauri wa Wizara ya Utalii. Kimsingi ni mwanamke mjasiriamali katika sekta mbali mbali za maisha na ni mwanachama hai wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Biashara kwa ajili ya kuwawezesha wanawake katika sekta binafsi.

Timor ya Mashariki
29 August 2020, 13:54