Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Chiara Porro kutoka Australia. Baba Mtakatifu Francisko amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Chiara Porro kutoka Australia.  (Vatican Media)

Papa Francisko Apokea Hati za Utambulisho wa Balozi wa Australia

Balozi Chiara Porro alizaliwa tarehe 30 Julai 1984, ameolewa na kubahatika kupata zawadi ya watoto wawili. Ni msomi aliyejipatia shahada ya uzamivu katika masuala ya siasa, falsafa na uchumi kutoka katika “University of York, Great Britain”. Baadaye alijipatia shahada ya uzamili katika masuala ya uhusiano wa kimataifa na diplomasia toka “University of Leiden, Netherlands, mwaka 2007.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 27 Agosti 2020 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Bibi Chiara Porro, Balozi mpya wa Australia mjini Vatican. Balozi Chiara Porro alizaliwa tarehe 30 Julai 1984, ameolewa na kubahatika kupata zawadi ya watoto wawili. Ni msomi aliyejipatia shahada ya uzamivu katika masuala ya siasa, falsafa na uchumi kutoka katika “University of York, Great Britain”. Baadaye alijiendeleza na hatimaye akafaulu kujipatia shahada ya uzamili katika masuala ya uhusiano wa kimataifa na diplomasia toka “University of Leiden, Netherlands kunako mwaka 2007.

Katika maisha yake ya kitaaluma, amewahi kuwa mfanyakazi katika Wizara ya Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa, Katibu, Ubalozi wa Australia nchini India na Ofisa mkuu mtendaji Australia huko Afrika Mashariki pamoja na Afrika ya Kati. Kati ya mwaka 2014-2015 aliteuliwa kuwa Afisa mtendaji wa Kikosi kazi cha Kupambana na Ugonjwa wa Ebola. Kati ya mwaka 2015 hadi mwaka 2016 alikuwa ni Kaimu mkurugenzi mkuu wa bajeti na programu za rasilimali fedha. Kati ya mwaka 2016-2018 aliteuliwa kuwa ni mshauri katika sekta ya ushirikiano wa kimataifa, Ofisi ya Waziri mkuu. Kati ya mwaka 2018-2020 amekuwa ni mshauri katika ubalozi wa New Caledonia, huko Noumèa. Mwishoni, kabla ya uteuzi huu, alikuwa ni Mkurugenzi wa kitengo kinachounganisha wizara mbali mbali nchini Australia.

Australia

 

 

29 August 2020, 13:43