Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Giambattista Diquattro kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Brazil. Kabla ya uteuzi huu alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini India na Nepal. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Giambattista Diquattro kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Brazil. Kabla ya uteuzi huu alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini India na Nepal. 

Askofu mkuu G. Diquattro: Balozi Mpya wa Vatican Nchini Brazil!

Askofu mkuu G. Diquattro alizaliwa tarehe 18 Machi 1954 huko Bologna. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 24 Agosti 1981 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 2 Aprili 2005 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Balozi wa Vatican nchini Panama na hivyo kumpandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu. Akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu, tarehe 4 Juni 2005.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Giambattista Diquattro kuwa ni Balozi mpya wa Vatican nchini Brazil. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Giambattista Diquattro alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini India na Nepal. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Giambattista Diquattro alizaliwa tarehe 18 Machi 1954 huko Jimbo kuu la Bologna, nchini Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 24 Agosti 1981 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Tarehe 2 Aprili 2005 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Balozi wa Vatican nchini Panama na hivyo kumpandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu. Akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu, tarehe 4 Juni 2005. Tarehe 21 Novemba 2008, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Bolivia. Tarehe 21 Januari 2017, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa ni Balozi wa Vatican nchini India na Nepal. Na ilipogota tarehe 29 Agosti 2020, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa ni Balozi mpya wa Vatican nchini Brazil.

Brazil
30 August 2020, 09:39