Kardinali Konrad Krajewski Mkuu wa Mfuko wa Kitume wa Papa atashughulikia usambazaji wa mahitaji ya lazima kwa maskini mjini Roma Kardinali Konrad Krajewski Mkuu wa Mfuko wa Kitume wa Papa atashughulikia usambazaji wa mahitaji ya lazima kwa maskini mjini Roma 

Vatican:Tani tano za mahitaji ya lazima kwa wenye hali ngumu mjini Roma!

Vatican imekabidhiwa tani 5 za mahitaji muhimu kwa ajili ya watu wasio na makazi maalum na familia mjini Roma ambao wamekabiliwa na umaskini zaidi kutokana na janga la virusi vya corona.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tani tano za vifaa na mahitaji muhimu kama vile pasta, mafuta, samaki za makopo (tuna), nyanya, maziwa, maharage vimetolewa zawadi kwa ajili ya kupelekwa kwa watu wasio na makazi lakini pia kwa maskini wapya kutokana na virusi vya corona. Ni msaada uliokabidhiwa mjini Vatican kwa Mkuu wa Mfuko wa sadaka ya Papa kutoka kwa Chama kisicho cha kiserikali kiitwacho “Moyo uliyoyeuka”, cha Toscana. Msaada huo ni kwa ajili ya, familia zote ambazo wakati wa karantini wameishiwa kila rasilimali na leo wanazidi kupata shida ya kuweka hata sahani kwenye meza. Aliyepokea msaada huo ni Mkuu wa  Sadaka ya Kitume  Kardinali Krajewski, ambaye amepokea  karibu tani 5 za mahitaji muhimu kwa ajili ya wale watu wanaoishi Roma katika hali halisi mbaya sana ya umaskini

Ni Malori meupe ya chama cha kiitwacho “Moyo unaoyeyuka”cha Toscana, kisicho cha kiserikali cha kutoa msaada kilichoanzisha miaka kumi iliyopita huko Florence (Firenze) Italia, lakini kinachofanya kazi nchini Italia kwa ujumla,ambapo magari hayo yalisimama katika Mlango wa Mtakatifu Anna ili kuingiza mjini Vatican na kukabidhi  zawadi hizi za msaada kwa Msimamizi wa Sadaka ya Kitume, na ambaye atasimamia utekelezaji wa usambazaji mjini kote Roma,  kama kawaida yake ya utume huu kwa wahitaji zaidi.

Umoja ni nguvu,  kati ya  Kardinali,  mkono wa kulia wa hisani  wa Papa na wa Chama hiki cha Mfuko ambacho, mara mbili kwa mwaka, huhamasisha watu wa kujitolea ili kukusanya maelfu ya bidhaa katika eneo lote nchini Italia, ambalo tayari limeonyesha ufanisi mkubwa katika utume wa kimisionari  kunako Desemba 2019 na Januari 2020. Kama kawaida yake Kardinali Konrad Krajewski atakwenda kwenye vituo vya Treni Roma kama alivyokuwa amefanya hata mwezi Machi katikati ya janga kuu zaidi na la karantini na kuendelea zaidi katika sehemu ambazo tayari zilikuwa na mateso na kuongezeka zaidi wakati huu wa janga la virusi.  

Kwa njia ya msaada huo, ni dhahiri kwamba wanaendeleza mshikamano na ushirikiano zaidi kati ya Vatican na chama hiki cha kilei na ambacho mwanzoni mwa mwezi Juni kilikuwa Hata kimesaidia familia zenye matatizo kwa fedha euro 120,000 za kununua zana. Hata hivyo ushirikiano huo utaendelea kwa miezi ijayo. Kama Papa asemavyo, katika kipindi hiki kigumu lazima kufanya kwa pamoja na siyo kufanya peke yetu kwa maana peke yetu hatuwezi.

23 July 2020, 15:31