Tafuta

Vatican News
Mlundikano wa wahamiaji wa ndani unahitaji kupatiwa suluhisho. Mlundikano wa wahamiaji wa ndani unahitaji kupatiwa suluhisho.  (ANSA)

VATICAN:Ask.Mkuu Jurkovič:Hitaji la ushirikiano kuhusu wimbi la ndani na zaidi walemavu!

Katika moyo wa hotuba ya wakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa huko Geneva ilikuwa ni juu ya Ripoti Maalum kuhusu Watu waliohamishwa ndani na kutazama kwa namna ya pekee watu walio hatarini zaidi miongoni mwao wenye ulemavu.Vatican inaamini kuwa ni muhimu kuzingatia mahitaji ya wenye ulemavu,ili usalama wao uhakikishwe na ushiriki wao kamili katika maisha ya jamii za wenyeji wao.

Na Sr. Angela Rwezaula;-Vatican.

Vatican ninaamini katika ushirikiano wa dhati na jumuiya ya kimataifa kuhusu shida za uhamisho wa watu wa ndani. Kwa lengo hili inahimiza ushirikiano wa mfumo uliowazi wa kisheria juu ya majukumu ya Mataifa ambayo yanahakikisha ulinzi wao mzuri, ili kupata suluhisho la kudumu na hatimaye kuokoa maisha ya wanadamu. Hayo yamebainishwa katika hotuba ya Askofu Mkuu Ivan Jurkovič, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa huko Geneva, akizungumza tarehe 9 Julai 2020 karika Kikao cha 44 cha Baraza la Haki na Amani kinachoendelea hadi tarehe 17 Julai kwenye mji wa Uswiss.

Watu walio hatarini zaidi miongoni mwao ni wenye ulemavu

Katika moyo wa hotuba hiyo ilikuwa ni juu ya Ripoti Maalum kuhusu Watu waliohamishwa ndani na kutazama kwa namna ya pekee watu walio hatarini zaidi miongoni mwao wenye ulemavu. Kama wahamiaji na wakimbizi, pia watu hawa ni ambao wanalazimika kukimbia ardhi zao, lakini wanabaki ndani ya Nchi zao, kwa maana hiyo mwakilishi wa kudumu wa Vatican amekumbusha kuwa hata hao ni waathirika wa kile kiitwacho “utandawazi wa sintofahamu” ambayo mara nyingi Papa Francisko amendelea kusema.

Watu waliolundikana ndani wanateseka sana

Watu waliohamishiwa ndani leo hii ni wahusika wakuu wa “janga lisiloonekana” na ambalo katika janga la Covid-19 limezidisha kama inavyoonyeshwa katika  Ujumbe wake wa Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi 2020 wa Papa Francisko”. Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Jurkovič ameongeza kusisistiza maneno ya ujumbe huo kuwa “wahamiaji na wakimbizi, watu waliohamishwa siyo idadi au takwimu kiurahisi kwa maana hawa ni watu na wana historia, mateso na matarajio binafsi”. Mateso mabaya ni kwa wale ambao wana ulemavu ambao hukutana na shida kubwa zaidi katika kupata habari na msaada kibinadamu na ukosefu wa usawa na hatari kubwa kwa ulinzi wao.

Ni muhimu kuzingatia mahitaji ya  wenye ulemavu,usalama wao uhakikishwe

Kwa sababu hizo, katika kusaidia watu waliohamishwa ndani, Vatican  inaamini kuwa  ni muhimu kuzingatia mahitaji ya wenye ulemavu, ili usalama wao uhakikishwe na ushiriki wao kamili katika maisha ya jamii za wenyeji wao  kama inavyopendekezwa na  “Miongozo ya kichungaji juu ya Watu waliohamishwa wa ndani” iliyoandaliwa na  Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Watu.  Ili kufikia hili Askofu Mkuu Jurkovič  amesema kuna ulazima wa ahadi za jitihada za nguvu kwa upande wa  Mataifa, mifumo ya uratibu zaidi na majukumu wazi ikizingatia kanuni kwa mujibu kwamba, watu wote, bila kujali hali yao ya wahamiaji na wanapaswa kubaki katika nchi zao kwa amani na usalama bila tishio la kuhamishwa tena. Lakini mifumo hii ya  kisheria peke yake haitoshi kwani  utashindwa ikiwa itaendelea na hukumu za utamaduni wa kukosa usawa na kuacha watu wengi nyuma.

10 July 2020, 09:21