Tafuta

Vatican News
Siku ya Bahari  Siku ya Bahari  

Mtazamo wa Kanisa kwa wafanyakazi wa baharini ambao hawawezi kurudi nyumbani!

Kanisa liko mstari wa mbele hata katika utume wa bahari na zaidi kwa wafanyakazi ambao hawawezi kurudi nyumbani kwa wakati huu wa kipindi kigumu cha virusi.Mtazamo huo unaoneshwa hata wakati wa fursa ya kuadhimisha siku ya utume wa bahari iliyofanyika tarehe 12 Julai 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula;-Vatican.

Wafanyakazi baharini mara nyingi wanalazima kukaa mbali na nyumbani, katika hali ngumu, wakiwa na mikataba ya kazi ambayo inaonyesha utumwa, na ukosefu wa kutoona ardhi kwa kipindi kirefu. Kwa sasa katika kipindi cha virusi vya corona, imebidi kuongeza muda wa wa kazi na kubaki zaidi kwa muda mrefu mbali na nyumbani kwao, kutokana na vizingiti na kufungwa kwa mipaka, na wakati mwingine wamekumba hata na utelekezwaji wa mambukizi. Ni kwa mujibu wa Kardinali Turkson katika ujumbe wake unaongazia watu hawa ambao karibu wanasahauliwa na kwa bahati nzuri Kanisa Katoliki linawakumbuka kupitia utume wa Baharini wa kitengo hiki cha Baraza la kipapa. Siku ya Bahari imeadhimishwa Jumapili tarehe 12 Julai 2020. Wazo la siku hii kwa mwaka huu lilikuwa ni kuadhimisha huko Glasgow, mahali ambao miaka 100 iliyopita yaani kunako mwaka 1920 iliona mwanzo wa utume wa Bahari ambao ulichukua jina la utume wa bahari kwa Wajesuit.

Mwanzo wa utume wa bahari

Ilikuwa ndiyo mwanzo wa kikundi cha walei na miongoni mwao hata waanglikani walioongekea ukatoliki na kufikiri kuanzisha muundo kwa jitihada kwa ajili  ya mabaharia. Mwamko wa kuanzisha huko ukawa sehemu ya jitihada rasmi ya Vatican ambao kwanza katika Baraza la makardinali kwenye miaka ya hamsini na baadaye kwenye Baraza la kipapa la wahamiaji hata kwa waraka wake binafsi motu proprio wa Mtakatifu Yohane Paulo II na hatimaye sasa, ambapo utume huo upo mikononi mwa Baraza la Kipapa la huduma ya Maendeleo Fungamani ya watu. Tendo la kutoadhimisha sherehe hizi huko Glasgow ni kutokana na janga la virusi vya corona, ambapo vizingiti vya mipaka na karantini kwa mataifa mengi, mkutano wa maadhimisho ya miaka 100 umehairishwa hadi kunako mwaka 202.

Mabaharia wengi wamepoteza ajira

Kardinali Turkson katika ujumbe wake unasema wakati makampuni mengi yamefungwa, viwanda vya baharini vinaendelea kufanya kazi na kuongeza changamoto nyingi za maisha ambazo kwazo zilikuwa tayari ni kwa watu ambao wanafanya kazi baharini na kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya virusi. Ikiwa meli hizi zinasafirisha asilimia 90 za bidhaa ambazo ni msingi wa kuendelea kuishi kawaida, kama vile madawa na vifaa vya matibabu, wakati huo meli hizo katika kusimama kwake, imekuwapo na ukiritimba  na serikali ili kuweza kushusha kwa usalama wageni na ambao wamekuwa wakipambana na virusi ndani ya Meli hizo. Lakini mabaharia hawakufikiriwa licha ya nafasi msingi ambayo wamekuwa nayo na matatizo ambayo wamekabiliana nayo. Kwa sababu katika hali hii wanafanyakazi wote ambao walikuwa tayari wamekwisha kaa miezi sita na miezi kumi ndani ya meli hizo imebidi wasubiri muda mwingine huku wakifanya kazi na matokeo kuongezeka ugumu binafsi na ukosefu wa ukaribu wa ndugu zao, wa kuwatia moyo katika nyumba zao. Ni karibia mabaharia 100,000 ambao kila mwezi wangeweza kurudi nyumbani mwishoni mwa mkataba wao na hawakuweza kufanya hivyo kutokana na dharura ya covid-19 na wakati huo huo idadi hiyo hiyo walikuwa tayari kubadilishana lakini hawakuweza na kubaki bila kazi.

Usalama ni suala muhimu na kusindikizwa kiroho

Baadhi ya wengine wamefika hatua ya kujiua kwa sababu wasingeweza kushuka katika nchi kavu, hata kuweza kupata wa kuwatembelea na wengine wameugua na wale ambao walikwenda kuwatembelea kwa ajili ya tiba waliwakuta katika hali mbaya na wengine walioweza kurudi, walitakiwa kukaa karantini tena au hata kubaguliwa. Yote hayo kwa mujibu wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo fungamani ya Watu wanabaini wakati wamiliki wa meli na wasimamizi wasiofaa, na   bila kuwa na moyo walitumia udhuru wa kubatilisha majukumu yao kwao, huku wakikataa kuhakikisha haki zao za kufanya kazi, mishahara ya kutosha na uhamasishaji wa mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wote. Usalama ni suala muhimu kwani katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 2020, mashambulio na majaribio ya kuteka nyara kutokana na maharamia yaliongezeka kwa asilimia 24%. Wengi, watapoteza kazi yao na ndiyo maana Jumapili ya bahari imewakumbuka hata hao Kardinali Turkson amebainisha.

Chama cha kujitolea cha Stella Maris

Katika ujumbe wake Kardinali anawakumbusha kuwa mabaharia hawako peke yao, kwa sababu makasisi na watu wa kujitolea wa Maria Nyote ya Bahari “Stella Maris” wako na pamoja nao mahali popote walipo na  sio muhimu kuwa wako kwenye  kilima cha kilemba bali  kupitia kwa makasisi kwenye mitandao ya kijamii ambayo inaendelea kusaidia mawasiliano na hawa wako tayari kila wakati kujibu simu yao, kutoa sikio lenye huruma na kuwaombea wema wao  na usalama wa familia zao. Kadhalika amekumbuka kwamba hakuna mtu atakayewaacha: makasisi na wanaojitolea wa Stella Maris ambao watakuwa na wao katika miezi ijayo, wakati uwezo wao utawekwa katika majaribu, na watajaribu kujibu mahitaji yao ya kimwili na ya kiroho. Watakuwa karibu na wao kila wakati, ili kupunguza wasiwasi wao, kutetea kazi yao na haki zao na kupigania dhidi ya  ubaguzi kwa maana hiyo wahisi kwamba wao siyo peke yao. Kadinali pia amesema kwamba hata lengo la  maombi la Papa Francisko  mnamo mwezi Agosti ijayo itakuwa kwa ajili  ulimwengu wa mabaharia. Katika maombi hayo yanaongezea na yake ya Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo fungamani ya watu mwaka huu yalitolewa kwa ajili ya Mama Maria wa Nyota ya Bahari(Maria Stella Maris).

14 July 2020, 14:31