Tafuta

Vatican News
2020.07.10 Tangazo la kushirikia mkutano kwa njia ya mtandoa kwa ajili ya kushehereka miaka 70  ya idhaa  ya Kingereza Afrika 2020.07.10 Tangazo la kushirikia mkutano kwa njia ya mtandoa kwa ajili ya kushehereka miaka 70 ya idhaa ya Kingereza Afrika  

Radio Vatican inaadhimisha miaka 70 ya matangazo ya kingereza barani Afrika!

Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican,Dkt.Paolo Ruffini atakuwa mgeni rasmi katika mkutano kwa njia ya mtandao uliondaliwa na Idhaa ya Kingereza Afrika,Ijumaa tarehe 17 Julai 2020.

VATICAN

Miaka 70 ya matangazo katika lugha ya kingereza barani  Afrika ni muhimu ambapo Radio Vatican inajiandaa kusheherekea tarehe 17 Julai 2020. Maadhimisho hayo yatafanyika kwa njia ya mtandao  kwa ushiriki wa Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican, Dk. Paolo Ruffini; Padre Federico Lombardi, SJ, Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Radio ya Vatican; Askofu Emmanuel Badejo wa Nigeria, anayewakilisha Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika na Madagacar(Secam) na washiriki wengine wa mawasiliano katoliki wa Kingereza. Zaidi ya hayo, hata mada kutoka kwa  Mama Mkuu Maria Claude Oguh, ambaye ni rais wa Baraza la Watawa wa Nigeria, na Sheila Pires, Mwendesha vipindi vya habari vya Radio Veritas Afrika  Kusini na mshiriki wa Radio Vatican.

Ushirikiano wa Radio Vatican na Signis

Kwa mujibu wa tukio hili liliondaliwa  na Signis Afrika na Idhaa ya Kingereza Afrika ya Radio Vatican, litaanza  saa 8.00 mchana masaa ya Ulaya kupitia mtandao kwa kuongoza na mada: “Hadithi kama zana ya  kukabiliana na shida za ubaguzi na za kijamii barani Afrika.” Kwa njia hiyo  itawezekana kufuatilia tukio hili moja kwa moja kwenye YouTube ya Radio Vatican  ya Kiingereza au kwenye ukurasa wa tovuti ya kingereza ya Vatican News.

Akielezea mpango huo, Padre Paul Samasumo, mkuu  wa Idhaa ya Kingereza Afrika, amesema kuwa “kwa  kuzingatia wakati mgumu wa sasa, imeonekana kufanya zaidi namna hii sherehe na tafakari”.  “Signs, ameongeza kusema ni Chombo Katoliki Ulimwenguni cha wataalam wa mawasiliano na ambacho kipo katika mabara yote.  Kwa maana hiyo tumemua kushirikiana nao ili kuwakaribisha katika mkutano kwa njia ya mtandao”. “Tulikuwa tunaweza kuchagua  kuzungumza sisi wenyewe kama mpango wa lugha za Radio Vatican, ameeleza tena Padre  Samasumo, lakini  labda bado kuna mambo mengine zaidi ya kutafakari pamoja juu ya matukio ya ulimwengu ambamo sisi tunaishi. Tunafurahi kuwa Rais wa Baraza letu yupo pamoja na sisi na vile vile uwepo wake Padre Lombardi ambaye haitaji kuwakilishwa”.

Mchango wa kusaidia maono ya mstakhabali wa Afrika

Kwa mujibu wa mada iliyochangulia, Padre Samasumo amebainisha kuwa “pamoja na Profesa, Padre Walter Ihejirika, kwa sasa ni Rais wa Signis Afrika na wengine tuligundua kuwa kama watangazaji  Katoliki barani Afrika, tuna jukumu ambalo si tu  kuripoti matukio ya kijamii, lakini  pia kusaidia jamii kutafuta njia ya maisha yaliyo bora ya wakati ujao. Mkutano huu kwa njia ya mtandao ni juhudi yetu ndogo kwa ajili ya kusaidia kutoa ramani ya mchakato wa safari kwa ajili ya mustakabali huu wa Afrika na ulimwengu kwa jumla”. Kwa njia hiyo, Padre Samasumo amesisitiza kuwa, wazo la kuanzia ni kutoka katika Ujumbe wa Papa Francisko  wa  Siku ya 54  ya Mawasiliano ya kijamii duniani  ili kuchochea akili za wanahabari Katoliki wa Kiafrika katika kazi hii muhimu ya kujenga bara lililo hai." Vile vile Padre Samasumo amesema “Ikiwa tutawasilisha ujumbe wa Injili kwa njia ya ubunifu na chanya, tunaweza kuchangia, kwa njia fulani, kuinua Afrika kutoka katika majivu ya shida, kutoka katika mizozo isiyo isha ya kisilaha na kutoka katika umaskini na ubaguzi ili  kuwa na maono ya kuelekea kwenye mustakabali wa ustawi na ujumuishaji wa kijamii” na zaidi  ameongeza kusema kwamba “mbele ya kukabiliwa na changamoto hizi, kiukweli, mwasilishaji katoliki hawezi kuruhusu kubaki kandoni.”

Radio Vatican kwa sasa ina umri wa miaka 89

Radio Vatican ilizinduliwa na Papa Pius XI kunako tarehe 12 Februari 1931, kwa maana hiyo ni miaka 89 sasa. Kipindi kwa jumla  cha lugha ya Kiingereza kilizinduliwa kunako 1937 na wakati kipindi maalum cha Kiingereza kwa upande wa Afrika kilizinduliwa mnamo 1950. Kunako mwaka  1979, kilitoka idhaa ya Kiingereza ulimwenguni  na kuundwa idhaa ya Kingereza Afrika kama inavyojulikana leo hii. Wazo hilo, kwa mujibu wa Sean Patrick Lovett, wakati huo akiwa ni mhusika mkuu wa Idhaa ya Kingereza ulimwenguni, lilikuwa ni kujibu mabadiliko ya mwenendo wa bara la Afrika. Vipindi vya Kingereza kwa upande Afrika vilianza kutangazwa jioni katika masafa mafupi.

Ushirikiano wa Radio Vatican na Radio nyingine katoliki Afrika

Redio ya Vatican inashirikiana na vituo vingi vya redio za majimbo na redio za kidini katoliki barani Afrika, ambazo zinatangaza katika vipindi vyao vya kila siku kwenye masafa yao ya FM. Kuna Podcast ya bure ya vipindi kwa sauti ya kila siku inayopatikana kila jioni kwenye ukurasa tovuti ya Kiingereza ya  Vatican News mahali ambapo pia kuna sehemu maalum ya habari za Kanisa barani Afrika, kwa njia nyingine, habari na maoni ya Kanisa la Afrika na kwa Kanisa ulimwengu zinapatikana!

11 July 2020, 15:00