Madhabahu ya Bikira Maria wa lourdes-Ufaransa Madhabahu ya Bikira Maria wa lourdes-Ufaransa 

Lourdes:Kardinali Parolin ataongoza Misa tarehe 15 Agosti!

Kardinali Pietro Parolin,Katibu wa Vatican anatarajia kwenda Lourdes tarehe 15 Agosti 2020,ili kuongoza Misa katika Siku kuu ya Kupalizwa mbinguni Mama Maria.Kabla ya kuelekea Lourdes,Kadinali atapitia katika mji wa Ars ujulikanao sana wa Mtakatifu Yohane Maria wa Vianey.

Na Sr. Angela Rwezaula

Kwa mujibu wa mwaliko kutoka kwa waandalizi ya hija kitaifa, Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican anatarajia kusafiri kwenda katika Madhabahu ya Mama Maria wa  Lourdes Ufaransa ili kuongoza  Ibada ya Misa Takatifu  katika Siku kuu ya Kupalizwa  Mbinguni Bikira Maria tarehe 15 Agosti 2020. Hata hivyo Kardinali Parolin alikuwa amepewa mwaliko katika madhabahu hiyo kabla ya kuibuka kwa virusi vya Corona japokuwa ameweza kuthibitisha ushiriki wake kunako Jumatatu hii. Kwa sababu ya vizuizi vinavyohusiana na janga la covid, Hija ya kitaifa mwaka huu itafanyika bila uwepo wa waamini ambao ni wagonjwa. Lakini wote wanaalikwa kuungana kiroho na tukio hilo kwa kufuatilia Misa kwa njia ya mtandao wa moja kwa moja. Licha ya mpango huo kubadilishwa, Katibu wa Vatican anafanya safari hiyo kwa ajili ya kuunga mkono Madhabahu ya Maria ambayo imeathiriwa sana na mgogoro wa sasa wa kiafya.

Aidha hii itakuwa safari ya kwanza rasmi nje ya Italia kama mwakilishi wa Vatican tangu janga hili kuanza. Kabla ya kufika Lourdes, Kardinali Parolin anatarajiwa kusimama katika jiji la Ars, mji  unaojulikana sana wa Mtakatifu Yohane  Maria wa Vianney. Ni safari yake ya tatu ya kwenda Lourdes tangu kuteuliwa kwake kama katibu Vatican  kunako 2013. Na kunako  2017 kama mwakilishi wa Papa katika Siku ya Wagonjwa Duniani na mnamo 2018 katika fursa za siku za  Mtakatifu Francis wa Sales.

Kardinali Parolin katika mji wa Mtakatifu Yohane Maria wa Vianey

Kwa mujibu wa Msimamizi wa Madhabahu ya Ars,Padre a Patrice Chocholski mesema kunako tarehe 4 Agosti katika fursa ya Siku kuu ya Mtakatifu Maria Yohane Vianey,e Kardinali ataongoza Misa Jumanne tarhe 4 Agosti 2020,  saa 4.00 asubuhi kabla ya kwenda kwenye mkutano mchana saa 9 alasiri unaohusu mada “Papa Francisko na makuhani katika safari na watu wa Mungu”. Katibu wa Vatican amealikwa katika madhabahu hiyo ya kifaransa ambapo siku hiyo anatarajia kuzindua mchakato wa historia ndani ya madhabahu kwa heshima ya ya   Kardinali Emile Biayenda, Askofu Mkuu wa Congo Brazzaville aliyefariki kunako  1977 na ambaye mchakato wa kutangazwa mtakatifu unaendelea  

Uhusiano uliopo wa kiongozi wa Congo katika madhabahu ya kifaransa unaanzia mbali katika kipindi cha mafunzo yake ambapo alikuwa akisomea Lion. Na alikuwa akienda kawaida huko Ars kwa kuwa ni karibu ili kujifunza zaidi tasaufi ya mtakatifi huyo wa Ars. Na alipokuwa akirudi toka Congo kituo cha kwanza kulikuwa ni katika madhabahu hiyo ya kifaransa. Padre Chocholski kwa maana hiyo amefafanua kuwa, uwepo wa Kardinali zParolin katika uzinduzi wa historia ya kardinali Emile Biayenda unaruhusu kujua zaidi karama ya Mtakatifu wa Ars  yaana Yohane Maria, baada ya Mtaguso wa II wa Vatican katika tamaduni mbali mbalimbali na hivyo hata ile ya Afrika na kwa ajili ya Mapadre wa Karne ya XXI.

07 July 2020, 17:40