Tafuta

2020.07.06 Papa Francisko huko  Lampedusa (08-07-2013) 2020.07.06 Papa Francisko huko Lampedusa (08-07-2013) 

Kumbu kumbu ya miaka 7 tangu Papa kutembelea Lampedusa!

Tarehe 8 Julai 2020 saa 5-6 asubuhi majira ya Ulaya,Papa anatarajia kuadhimisha ibada ya Misa Takatifu katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican.ili kukumbubuka miaka 7 tangu atembelee Lampedusa mwaka 2013.Kutokana na hali halisi ya kiafya misa watakaoshiriki misa hiyo ni wahausika wa Kitengo cha Wahamiaji na Wakimbizi cha Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Watu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Licha ya kuwa na umakini wa kuzuia maambukizi ya Covid-19, lakini ni fursa isiyosahauliwa ambayo hata mwaka huu Papa Francisko amependelea kuionyesha kwa kuadhimisha Misa katika kukumbuka ziara yake huko Lampedusa katika Kisiwa ambacho kipo kati ya Tunisia na Italia kwenye bahari ya Mediterranea na Mkondo wa Kisiwa cha Sicilia. “Eneo hili badala ya kuwa njia ya matumaini, iligeuka kuwa njia ya vifo kwa maelfu na maelfu ya wahamiaji”. Kwa mujibu wa msemaji Mkuu wa vyombo vya habari Vatican, Dkt. Matteo Bruni amebainisha kuwa Jumatano tarehe 8 Julai 2020, kuanzia saa 5.00 hadi saa 6.00 kamili majira ya Ulaya, Papa Francisko ataadhimisha Misa Takatifu katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta ikiwa ni siku ya  kumbu kumbu ya miaka 7 tangu afanye  ziara yake huko Lampedusa mwaka 2013. Aidha kutokana na hali halisi ya kiafya na umakini wa kujikinga na maambukizi, watakaoshiriki misa hiyo ni wahusika wa Kitengo cha Wahamiaji na Wakimbizi cha Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Watu.

Mwaka 2019 misa ilifanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Pietro

Mwaka jana Papa Francisko aliadhimisha Misa hiyo katika Altare ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na kushiriki karibia watu 250 miongoni mwao wakiwa ni wakimbizi, wahamiaji na wale ambao wanajikita katika kuokoa maisha. Itakumbukwa safari yake  ya kwanza nje ya mji wa Vatican, Papa Francisko alipendelea kutoa sauti kwa kutangaza juu ya ‘utandawazi wa sintofahamu’ ambao unazuia watu wasijali vilio vya wengine. Papa Francisko anasimulia katika mahojiano ambayo yameelezwa katika kitabu kiitwacho “safari” cha Andrea Tornielli, kwamba alihisi na kuguswa na habari kuhusu wahamiaji waliokufa baharini, wakazama na ambao ni watu wa kawaida, watoto, wanawake, wanaume, ambao lakini bado wanaendelea kupoteza maisha hata leo, miaka saba baada ya safari hiyo, wakati wa kuvuka kwa mahangaiko na mara nyingi ndani ya boti zisizoaminika, ambazo zimekabidhiwa na kusimamiwa na watu wasiokuwa na adabu.

Siku chache  baada ya ziara yake tarehe 3 Oktoba likatokea janga tena

Katika ziara yake aliyofanya wakati huo, haikuwa katika ratiba yake na bila kuwa na mwaliko maalum, bali kwa kuongozwa na hisia ambazo alihisi kwenda, kwa mujibu wa maneno yake wakati wa mahojiano yake. Ilikuwa ni ratiba iliyopangwa kwa lisaa limoja na nusu, lakini ambalo lilitoa heshima kubwa kwa waathirika wa Bahari ya Mediterranea, kati ya manusura na wakazi wa visiwa vya Pelagie, Kanisa na taasisi mahalia, pamoja na mapadre na wahudumu wa kibinadamu. Katika mahubiri yake kwenye Uwanja wa michezo, mbele ya watu elfu kumi, ambao ulikuwa umeandaliwa vema kwa kutumia hata majabali ya mitumbwi ili kukukumbuka vifo vya wahamiaji wengi na wazo kama mwiba rohoni.  Safari ya Lampedusa kwa maana hiyo inaamsha dhamiri zetu tena  ili kile kilichotokea kisiweze kurudia tena. Lakini kwa bahati mbaya majanga ya wahamiaji waliokufa baharini huko Lampedusa si  hao tu bali hata baada ya miezi michache za kutembelea huko, tarehe 3 Oktoba mwaka huo huo, walikufa wengine 366. Na manusura wa janga hilo walipokelewa mwaka uliofuata na Papa Francisko mjini Vatican. 

Tumeangukia katika utandawazi wa sintofahamu

Katika sehemu ya ishara ya mateso kwenye Bahari ya Meditterranea, kilio cha Papa bado kinasikika katika ulimwengu huu wa utandawazi ambapo amesema "tumeangukia katika utandawazi wa kutojali, tumezoea mateso ya wengine na wala hatuyajali, hayatuwi na  huruma na wala hatuna uwezo wa kulia. Maombi yake yalikuwa wakati huo ni kumwomba “Bwana msamaha wa kutokujali kwa ndugu na dada wengi; msamaha kwa wale ambao wameketi chini kwa ustawi wao binafsi na kugandisha hisia za mioyo yao; msamaha kwa wale ambao kwa maamuzi wameamua kuunda mazingira kwa ngazi ya ulimwengu na ambayo yanasababisha majanga haya, ili ulimwengu uweze kuwa na ujasiri wa kuwakaribisha wale wanaotafuta maisha bora” na juu ya ‘utandawazi wa sintofahamu’ ambao unazuia watu wasijali vilio vya wengine.

06 July 2020, 14:57