Papa wakati anakutana na ndugu wahamiaji huko Lamedusa. Papa wakati anakutana na ndugu wahamiaji huko Lamedusa. 

Yuko wapi kaka yako?kutoka Lampedusa hadi Covid,changamoto ya udugu!

Baada ya miaka 7 tangu ziara yake katika kisiwa,Papa anarudia kutoa wito wa dharura na ili kuhisi kama ndugu wa kusaidiana mmoja na mwingine.Jambo la udugu linaweza kuonekana zaidi wakati huu wa kipindi baada ya janga kwani hakuna uwezekano wa kujiokoa binafasi maana udugu ndiyo njia pekee ya kujenga wakati ujao.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Katika kilele cha kitimiza miaka saba tangu Papa Francisko atembelee kisia cha Lampedusa Dk. Alessandro Gisotti Kaimu Mhariri wa Baraza la Kipapa la Maawasiliano katika makala yake anajikita kufafanua nini maana ya udugu katika matendo ya utume wa Papa Francisko. Akienza kufafanua anaandika “Ndugu yako yuko wapi? Sauti ya damu yake imepaza kilio hadi kwangu kwamba anasema Mungu. Hilo ndilo swali ambalo linawageukia wengine, ni swali ambao linageukia mimi, wewe, na kila mmoja wetu”. Imepita sasa miaka saba tangu Papa Francisko afanye ziara yake fupi huko Lampedusa  na wakati huo kuna swali ambalo aliwauliza watu wakati wa  misa aliyoadhimisha kwenye kiwanja cha mpira katika kisiwa kilichopo kwenye moyo wa Mediterraneo.  Ni safari iliyodumu masaa machache lakini ambayo kwa namna moja iliweza kuonesha bayana mpango mzima wa utume wa Papa. Pale katika nchi  ya Kusini mwa Ulaya, Papa Francisko alionyesha nini maana anapozungumzia “Kanisa la kutoka nje”! Alifanya kuonekana uthibitisho ambao hali halisi unatazama vizuri pembenzoni kuliko sehemu za katikati. Akiwa katikati ya wahamiaji waliokimbia vita na hali ngumu ya maisha, aliweza kugusa kwa mkono wake ndoto yake ya “Kanisa maskini kwa ajili ya maskini”. Huko Lampedusa, kwa upande mwingine, akizungumzia juu ya Kaini na Abeli, aliweka nafasi ya kwanza hata mpango wa kujiuliza juu ya udugu. Na ni swali msingi kwa ajili ya wakati wetu au labda kwa kila wakati. Katika msingi wa Udugu, unazungukia huduma ya Kipapa. Hata hivyo “Ndugu’, ndilo lilikuwa neno lake  la kwanza kutamka akiwageukia  ulimwengu usiku wa tarehe 13 Machi 2013, anaandika Dk. Gissoti.

Thamani ya udugu kama ndiyo hivi inawezekana kusema kwamba  iko katika damu ya Papa aliyechagua jina la “Maskini mdogo wa Assisi, mtu ambaye kwa upendo wake alijiit jina la mdogo  yaani ndugu. Vile vile udugu pia ni namna anavyojifafanua katika uhusiano wake na Papa Mstaafu Benedikto XVI. Baada ya sahini ya Hati ya Udugu wa Kibinadamu, maelezo hayo yanajionesha wazi kwa wote. Na zaidi kwa kutazama mchakato wa kwa miaka 7 ya  nyuma  katika upapa wa Papa Francisko yameonekana matendo msingi yaliofikia kutia sahihini pamoja na Imam Mkuu wa  Al Azhar, katika Hati ya kihistoria huko Abu Dhabi, kunako tarehe 4 Februari 2019. Mchakato huo sasa unaendelea kwa sababu matukio katika Dunia ya kiarabu yalikua ni mahali pa kufikia lakini pia ni kituo cha kuanzia, anabainisha Dk Gisotti. Kwa kurudi kwenye swali la Lampedusa, kwa namna ya pekee Papa alitumia maneno yale yale katika ziara nyingine yenye ishara ya nguvu, aliyofanya huko Puglia wakati wa fursa ya kukumbuka miaka 100 tangu mwanzo wa vita ya Kwanza ya Dunia.

Hata hivyo hata  kunako Septemba 2014, ilisikika sauti ile ya mazungumzo kati ya Mungu na Kaini, baada ya kumuua ndugu yake Abeli. Na yeye akijibu kuwa ananihusu nini? Kwani mimi mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? (Mw 4,9).  Kwa upande wa Papa, anathibitisha kwamba tendo la kukataa kuwa mlinzi wa ndugu, kila ndugu, ndiyo mzizi wa mabaya yote ambayo yanamkumba binadamu. Tabia hii, Papa anasisitiza ni kinyme na yale asemaye Yesu katika Injili kuwa “anayemjali ndugu anaingia katika furaha ya Bwana; ambaye hafanyi hivyo na kutotimiza wajibu ni wazi   anabaki nje”. Kwa maana hiyo katika mchakato wa safari hiyo, tunaona huduma ya Papa katika mambo ambayo yanaendela sambamba na udugu. Pamoja na mtiririko wa shughuli za huduma ya Kipapa tunaona kwamba udugu wa kibinadamu unazidi kupungua nguvu zake zote na ambazo zipo katika mitindo mbali mbali kama ile ya  kiekumene hadi kidini, kutoka katika  kijamii hadi ya kisiasa. Kwa mara nyingine tena, inazunguka sura hii ambayo kweli inawakilisha mawazo na hatua za matendo ya Papa Francisko. Kwa hakika  undugu una sura  nyingi kama hizo. Kwa kadiri watu walivyo wengi na uhusiano pia kati yao.

Papa alizungumza kuhusu ndugu katika Mkutano wa sala na amani katika Bustani za Vatican akiwa na Shimon Peres na Abu Mazen,  viongozi wa kisiasa alisema “ uwepo wenu ni ishara kubwa ya udugu ambao unastahili  kwa wana wa Ibrahim. Ni  kielelezo cha kweli cha imani katika Mungu, Bwana wa historia ambayo leo hii inatutazama kama mmoja na mwingine na shauku ya kutuongoza katika njia zake”. Kwa jina la udugu ulio hai na umoja wa imani katika Kristo ulitimizwa hata wakati wa mkutano ambao haukuwa unafikiriwa miaka ya kwanza kabla ya kuwa Askofu wa Roma akiwa na Patriaki wa Moscow, tukio kukutana  na Patriaki wa Costantinople, ndugu yake  Bartholomew I. Huko  Cuba, Papa Francisko na Kirill walitia sahini katika hati ya pamoja ambayo ilikuwa inasisitiza kwamba “kwa furaha tumejikuta kama ndugu katika imani kikristo ambao wanakutana ili kuzungumza kwa sauti iliyo hai”. 

Udugu vile vile ni neno kama ufunguo unaoturuhusu kuingia katika moja ya matendo yenye nguvu na kushangaza kwa utume wa Papa. Itakumbukwa ishara ya kupiga magoti na kubusu viongozi wa Sudan Kusini wakati wa mafungo yao ya kiroho na amani mjini Vatican. “ Ninyi watatu mmetia sahini ya makubaliano  ya amani, ninawaomba kama ndugu, mbaki katika amani. Ninawaomba kwa moyo wote. Twende mbele” aliwambia  Papa Francisko. Ikiwa tamko la Abu Dhabi lilikuwa kama ua la mbegu zilizopandwa mwanzoni na baadaye katika mchakato wa Kipapa kwa hakika “ mabadiliko ya wakati ambayo tunaishi na yaliyochochewa na janga, yanafanya kuchukua jukumu kulingana na masuala ya udugu kibinadamu

Yuko wapi ndugu yako, swali lile ni wito aliotoa tena kuna tarehe 8 Julai 2013 huko Lampedusa. Na leo hii ndilo swalili hilo katika ulimwengu unaoamini kuwa na uwezo wake, uwezo wa kwenda mbele na mantiki ya ubinafsi na kasumba za kwamba tumezoea kufanya hivyo, kwa sasa ulimwengu huo umejikuta imeanguka chini, bila kuamini, ulimwengu usio na nguvu mbele ya adui hasiyeonekana. Na sasa inakuwa ngumu katika kuamka na kutafuta nguzo nzuri ya kuegemea. Msingi huo kwa upande wa Papa anarudia ni udugu. Udugu ndiyo msingi pekee ambamo inawezekana kujenga nyumba imara kwa ajili ya ubinadamu. Papa Francisko alisema “sisi ni ndugu katika mtumbwi mmoja unao yumbishwa na mawimbi ya dhoruba ambayo imekumba wote na kila mmoja katika umbali wake.

Katika dhoruba hii, Papa Fracisko alisisitiza akiwa chini ya mvua iliyokuwa ikinyesha kunako tarehe 27 Machi 2020 katika Uwanja wa Mtakatifu Petro ukiwa wazi bila watu. Tazama  ni kitu gani kinaweza kuamsha dhamiri zetu kidogo mbele ya majanga mengi kama vile vita, na njaa kwa wale ambao wamebisha hodi milangoni petu lakini hatukuwaonea huruma na wala kuwaacha waingie ndani ya nyumba. Kuna majanga mengine mengi ambayo yanafanya watu wafe , alikumbusha pia Papa Francisko katika Misa ya Mtakatifu Marta tarehe 14 Mei 2020 . Na kwamba hatugutiki , badala yake tunageukia sehemu nyingine. Leo hii kama vila miaka 7 iliyopita huko Lampedusa,  Dk. Gissoti amehitimisha, Papa anasema kuwa hatupaswi kutazama upande mwingine kwa sababu ikiwa kweli sisi tunahisi kuwa ndugu kwa kushirikiana mmoja na mwingine basi, upande mwingine haupo kabisa,kwa maana upande mwingine ni sisi sote!

07 July 2020, 13:30