Colombia-Bi Gambino:Jukumu la kichungaji la familia na kizazi kipya!

Katibu msaidizi wa Baraza la Kippa la Walei,Familia na Maisha ametuma ujumbe kwa Baraza la Maaskofu wa Colombia wakiwa katika mkutano mkuu wa Mwaka.Shughuli za kichungaji kwa familia,zina changamoto kubwa mbele yake hasa katika kuonesha vizazi vipya kwamba familia haina ugumu na matatizo tu lakini pia ni furaha,wito na safari ya furaha.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kutazama kwa upya njia na yaliyomo katika kuandaa vijana na kuwasindikiza  katika ndoa zao kwa kuwafanya hawa wenzi wa ndoa wawe mstari wa mbele katika shughuli za kichungaji kwa familia na kuwasaidia wazazi katika kuelimisha watoto wao. Zaidi ya hayo, ni katika kutoa nafasi ya jitihada za shughuli za kichungaji kwa wazee na watu wadhaifu zaidi katika familia.

Hizi ndizo dharura za kichungaji kwa familia kwa mujibu wa Bi Gabriella Gambino, Katibu Msaidizi wa Baraza la kipapa la Walei, Familia na Maisha ambaye kwa njia ya video amewalekeza washiriki wa Baraza la Maaskofu nchini Colombia katika fursa ya Mkutano  mkuu wa mwaka.

Bi Gambino amesema “Shughuli za kichungaji kwa familia, zina changamoto kubwa mbele yake na  inabidi  kuonyesha kwa vizazi vipya kwamba  katika familia siyo kwamba kuna ugumu tu na matatizo,  lakini pia kuna furaha, wito na ni njia ya furaha” na mengine. Kwa kuongozwa na Wosia wa Kitume wa Papa Francisko, wa Amoris leticia amebainisha kwa kirefu umuhimu wa kujenga Kanisa kwa mchango mkubwa wa familia na katika kuelimisha watoto.

09 July 2020, 13:31