Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Msaidizi Benjamin Phiri kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Ndola, Zambia Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Msaidizi Benjamin Phiri kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Ndola, Zambia 

Askofu Benjamini Phiri, Jimbo Katoliki la Ndola, Zambia! Kumenoga!

Askofu Benjamin Phiri, alizaliwa tarehe 14 Juni 1959 huko Chongololo. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 14 Septemba 1986 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 15 Januari 2011, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Chipata. Kardinali Medardo Joseph Mazombwe, akamweka wakfu kuwa Askofu tarehe 9 Aprili 2011.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameteua Askofu Msaidizi Benjamin Phiri kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Ndola, nchini Zambia. Kabla ya uteuzi huu, Askofu Benjamin Phiri, alikuwa ni Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Chipata, Zambia. Itakumbukwa kwamba, Askofu Benjamin Phiri, alizaliwa tarehe 14 Juni 1959 huko Chongololo, Chipata. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 14 Septemba 1986 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Tarehe 15 Januari 2011, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Chipata. Kardinali Medardo Joseph Mazombwe, akamweka wakfu kuwa Askofu tarehe 9 Aprili 2011. Jimbo Katoliki la Ndola, limekuwa wazi kuanzia tarehe 30 Januari 2018, baada ya Baba Mtakatifu Francisko kumteua Askofu Alick Banda kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Lusaka na Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki la Chipata, Zambia.

Ndola: Zambia
03 July 2020, 13:43