Vatican.Ushuhuda wa Kard.Comastri:Sala ya Rosari imegusa wengi katika kipindi cha janga!

Yesu anabadilisha maisha hasa katika kukutana naye na wala haitaji jambo lolote.Sala ndiyo jambo zuri zaidi ambalo tunaweza kufanya katika maisha yetu.Watu wengi wameguswa na sala ya Rosari wakati wa janga la corona,kwa mujibu wa Kardinali Comastri ambaye ameongoza rosari na sala ya malkia wa Mbingu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kila siku kwa siku 66 katika kipindi kigumu cha janga.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Karibia milioni moja na nusu ya watu na maelfu ya barua ambazo zinaendelea kufika hadi leo hii mjini Vatican. Ni urithi wa sala ya rosari na Sala ya Malkia wa Mbingu ambayo Kardinali Angelo Comastri amekuwa akisali kila siku akiwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro wakati wa kipindi  kigumu cha janga la virusi vya korona saa sita na ambayo ilitangazwa moja kwa moja na vyombo vya habari. Ni wasikilizaji wengi wa ajabu ambao hakuna aliyekuwa anaweza kufikiria, kwa mujibu wa Kardinali ambaye amebainisha kuwa mashuhuda wengi wa imani wamegundua imani na wengine wapya ambao wamejiunga kusali sala  mara nyingi  katika hali ya kila siku. Tukio la sala limepata  kusambaa sana, shukrani kwa vyombo vya habari Vatican. Ni uzoefu ambao ulikuwa ufanyike kwa siku chache tu kuanzia tarehe 11 Machi na kumbe ukazaa wiki baada ya wiki, mwezi baada ya mwezi hadi kufikia mwisho wa mwezi Mei, lakini pia sala ilikatika kwa muda mfupi tu wa Juma Kuu Takatifu, ambapo kwa ujumla ni siku 66 za kusali kila siku Rosari Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro!

Sala inatuweka katika muungano na Bwana

Kardinali Comastri aidha amebainisha jinsi alivyohusika sana na matukio akikumbuka mialiko mingi ya kuendeleza mbele sala hizo. Kwa sasa anapoona kuanza kwa upya ukawaida wa maadhimisho ya misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kwake yeye anaona ugumu kidogo, lakini amesema kama inawezekana kutokea fursa ya hali nyingine , yeye yuko tayari kujikita katika kambi hiyo ya mwendelezo wa sala. Na hii amefafanua kwamba, sala inatuweka katika muungano na Bwana; na ndiyo ilivyojitokeza katika sala wakati wa siku za giza nene la janga la virusi vya corona.

Kumbu kumbu ya mama yake mzazi

Kardinali Comastri akielezea juu ya kumbu kumbu yake ya  mwisho ambayo ilikuwa ni siku ya mkesha wa tarehe 8 Mei hasa alipotamka  juu ya mama yake mzazi na kusema kuwa  “mama yangu alinisindikiza hadi nilipochaguliwa kuwa Askofu Mkuu wa Loreto. Yeye alikuwa aendi kitandani kabla mimi sijarudi nyumbani. Na alikuwa akifunga mlango wangu na kusema ‘ulale salama mwanangu na Bwana akubariki! Huyo ndiye mama! Anapokosekana mama katika maisha ya mtoto yanakuwa machungu, magumu na hata ya huzuni”, amefafanua Kardinali.

Uzuri wa wema

Katika hatua  zinazofuata baada ya dharura, Kardinali anabainisha kuwa ni lazima kuzingaitia akilini mafundisho kadhaa. Na hii ni kutokana na kwamba karibu kila mmoja amekuwa na unyenyekevu wa kutambua kuwa sisi siyo mabwana wa ulimwengu huu. Imetosha virusi visivyoonekana, kupigisha magoti utajiri wa uchumi wa Magharibi. Na ni matokeo mengi ambayo yapo katika uzoefu. Wengi wamegundua hata uziri wa kutenda wema, huku akikumbuka mapendekezo ya vijana wengi ambao walimsimulia juu ya  shauku zao za kuwasaidia wazee katika nyumba zao na katika mahospitalini.

Watu wanatafuta mapadre ili waweze kukutana na Yesu

Katika kujibu swali ni kwa namna gani uzoefu wa janga umembadili Kardinali Comastri amesema “ ninaweza kusema kwa uwazi na ukweli kuwa zaidi nimehakikisha ni jinsi gani watu wengi wanatafuta mapadre tu kwa ajili ya msaada wa kuweza kukutana na Yesu.  Yesu anabadilisha maisha hasa katika kukutana naye na wala haitaji jambo lolote. Sala ndiyo jambo zuri zaidi ambalo tunaweza kufanya katika maisha yetu”, amehitimisha Kardinali Comastri.

08 June 2020, 14:40