Kardinali Pietro Parolin ameteuwa wajumbe wa Tume ya Kipapa ya Shughuli ya Afya kuanzia Juni 2020 hadi Juni 2023. Kardinali Pietro Parolin ameteuwa wajumbe wa Tume ya Kipapa ya Shughuli ya Afya kuanzia Juni 2020 hadi Juni 2023. 

Wajumbe wa Tume ya Kipapa ya Shughuli za Afya 2020-Juni 2023

wajumbe wapya wa “Tume ya Kipapa ya Shughuli za Afya” watakaoshikilia nafasi hizi kuanzia mwezi Juni 2020 hadi Juni 2023.Tume hii itakuwa chini ya Monsinyo Luigi MISTO’, Rais wa Mfuko wa FAS. Wajumbe wengine ni Monsinyo Segundo Tejado Muñoz,: Prof. Renato BALDUZZI, Prof. Na Wakili Giovanni BARBARA; Prof. Saverio CAPOLUPO; Dr. Fabrizio CELANI; Dr. Maurizio GALLO.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwa mamlaka aliyokabidhiwa na Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 1 Juni 2020, amewateuwa wajumbe wapya wa “Tume ya Kipapa ya Shughuli za Afya” watakaoshikilia nafasi hizi kuanzia mwezi Juni 2020 hadi Mwezi Juni 2023.Tume hii itakuwa chini ya Monsinyo Luigi MISTO’, Rais wa Mfuko wa Bima ya Afya Vatican, FAS. Wajumbe wengine ni Monsinyo Segundo Tejado Muñoz, Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo endelevu na fungamani ya binadamu: Prof. Renato BALDUZZI, Prof. Na Wakili Giovanni BARBARA; Prof. Saverio CAPOLUPO; Dr. Fabrizio CELANI; Dr. Maurizio GALLO.

Wakati huo huo, Kardinali Parolin amemteua Padre Marco BELLADELLI, Mshauri wa Shirikisho la Wafamasia Wakatoliki Italia, kuwa Mkurugenzi wa Ofisi ya Tume ya Kipapa ya Shughuli za Afya. Atakuwa na sauti pamoja na haki ya kupiga kura ya maamuzi katika Tume hii ya Kipapa. Kwa upande mwingine, Sr. Annunziata REMOSSI, 0.M.V.F., Afisa kutoka Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume, ataendelea kuwa Katibu mkuu wa Tume hii kwa kipindi cha miaka mitatu. Tume hii inaweza kufanya mikutano yake mara kwa mara kadiri itakavyoonekana inafaa au kutokana na ushauri wa kifundi au kutoka kwa wakuu wa Sekta ya Afya. Ni matumaini ya Kardinali Parolin kwamba, wajumbe wataweza kutumia uzoefu na mang’amuzi yao kusaidia mchakato wa maboresho katika huduma ya afya, kwa kuwachagua watu wachache wanaoweza kuchangia mawazo.

Kardinali Parolin, ametumia fursa hii, kuwashukuru wajumbe waliomaliza muda wao kwa huduma, ukarimu na upendo waliouonesha katika maisha na utume wa Kanisa. Kwa sasa, ni wakati wa kufungua ukurasa mpya kwa kuwapatia wajumbe wengine nafasi ya kuweza kuchangia zaidi katika mchakato wa huduma ya afya duniani. Mabadiliko haya muhimu ni sehemu ya mang’amuzi ya huduma ya Kanisa Katoliki inayotolewa sehemu mbali mbali za dunia chini ya uongozi wa Baba Mtakatifu Francisko. Kardinali Parolin anawashukuru na kuwapongeza kwa mchango na huduma yao makini na hasa katika kipindi hiki cha janga kubwa la homa kali ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona, COVID-19.

Tume ya Kipapa ya Afya
16 June 2020, 14:29