2020.06.18 Papa Benedikto XVI na kaka yake Georg Ratzinger 2020.06.18 Papa Benedikto XVI na kaka yake Georg Ratzinger  

Papa Mtaafu Benedikto XVI nchini Ujerumani kumwona kaka yake mgonjwa!

Kwa kupendelea kuwa karibu na kaka anayeumwa Papa mstaafu amefika leo hii huko Regensburg,Ujerumani.Pamoja na Papa mstaafu Benedikto XVI ameambatana na Monsinyo Gaenswein,Makamu Mkuu wa Kikosi cha Ulinzi jijini Vatican na kikundi cha kiafya na wahudumu.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Safari ya kwenda Ujerumani kutoka katika sehemu yenye ukimya katika Monasteri ya Mater Ecclesiae mjini Vatican hadi Regensburg, ili kuwa karibu na mwenye umri wa miaka 96 ambaye anaumwa. Hii ni safari iliyotimizwa asubuhi na Papa Mstaafu Benedikto XVI ambaye ameacha mahali anapoishi na kufikia nchi yake Ujerumani, kwa kusindikizwa na Monsinyo Georg Gaenswein, Daktari na wahudumu mbali mbali wa afya, pamoja na Makamu mkuu wa kikosi cha Ulinzi wa mji wa Vatican. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jimbo la Regensburg, Papa Mstaafu ametua Monaco ya Baviera saa 5.45 asubuhi na kupokelewa na Askofu Rudolf Voderholzer na ambaye amemsindikiza huko Regensburg.

Papa mstaafu Benedikto XVI kwa mujibu wa yaliyothibitishwa na msemaji wa vyombo vya habari Vatican, Dr. Matteo Bruni, atabaki nchini Ujerumani kwa muda wa lazima katika seminari ya jimbo la Regensburg.  Jimbo lenyewe la limewaalika waamini kuheshimu kipindi na kwa mujibu wa utashi wa ndugu hao wawili, kuacha kwamba mkutano huo binafsi wa kina ubaki faragha bila kuonekana kwa umma.

Katika fursa ya kufika kwa Papa mstaafu Benedikto XVI nchini Ujerumani, Rais wa Baraza la Maaskofu Ujerumani Askofu Georg Bätzing, amethibitisha juu ya kutaka kumsindikiza kwa sala zake kwa siku ambazo Papa atakuwa na kaka yake Georg. “Tunayo furaha kwamba yeye ambaye alikuwa mmoja wa Baraza letu la maaskofu kwa miaka kadhaa, amerudi tena nyumbani, hata kama ni wakati wa huzuni."

Ndugu wawili hawa Ratzinger wamekuwa na muungano kati yao waliotenganisha na umri wa miaka mitatu tu, walipewa daraja la Upadre katika siku moja tarehe 29 Juni 1951, katika Kanisa Kuu la Freising. Katika mazingira ya maisha yamewaelekeza katika mwelekeo tofauti, kwani Georg ni mwanamuziki mzuri, Papa Joseph ni Mtaalimungu wa kiwango cha juu,  lakini wakiwa na dhamana ya kuheshimiana daima na ambayo imekuwa yenye nguvu. Uthibitisho huo unaoneshwa wazi hasa katika ziara nyingi ambazo Georg Ratzinger amezifanya kuja jijini Vatican, tangu 2005 hadi 2013, katika miaka ya Upapa wa kaka yake hata baada ya kustaafu kwake.

Kunano mwaka 2008  katika jiji la Castel Gandolfo alipendelea kutoa uraia wa heshima kwa kaka yake na Papa Msatafu Benedikto XVI alielezea kwa maneno haya: “Tangu kuzaliwa, kaka yangu amekuwa siyo rafiki yangu tu, bali pia kiongozi wa kuaminika. Amekuwa akiwakilisha hatua ya mwelekeo na kumbukumbu kwa uwazi na uamuzi wa maamuzi yake”. Ni maneno ya upendo mkubwa, uliozaliwa katika hali ya kufurahi na ambayo hisia za wakati huu zinaonekana hata zaidi.

18 June 2020, 18:05