Tafuta

Vatican News
Vifaa vya kusaidia kupima maambukizi ya virusi viliwasilishwa na Caritas ya Yerusalem huko kwa paroko wa parokia ya  Familia Takatifu huko Gaza Vifaa vya kusaidia kupima maambukizi ya virusi viliwasilishwa na Caritas ya Yerusalem huko kwa paroko wa parokia ya Familia Takatifu huko Gaza 

Mshikamano wa Papa wa vifaa vya kiafya umefika Gaza!

Papa Francisko ametoa mchango wa mshikamano kwa vipimo 2,500 vya Covid-19 katika Wizara ya Afya huko Gaza,kupitia Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki.Uwasilishaji wa vifaa hivyo uliratibiwa na Uwakilishi wa kitume na Patriaki wa Kilatino huko Yerusalem na Caritas ya Yerusalemu,tarehe 17 Juni 2020,kwa mujibu wa upatriaki huo.

Na sr. Angela Rwezaula- Vatican

Hadi sasa ni kesi 1284 za maambuzi ya Covid19 katika ukanda wa Gaza lakini inawezekana kesi kuwa kubwa zaidi kutokana na kukosa vipimo. Paroko wa Gaza Padre Romanelli amesema  hayo kwamba vifaa vilivyo tumwa na Papa  Francisko vitasaidia kufanya uchunguzi makini. Katika ukanda wote wa Gaza kuna mashine moja tu ambayo inaweza kupima kwa zaidi ya watu milioni  2.  Shukrani zinamwendea Papa ambaye ametoa mchango wake wa mshikamano kwa vipimo 2500 vya Covid-19 katika Wizara ya Afya huko Gaza, kupitia Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki. 

Sura nyingi za upendo wa Papa

Uwasilishaji wa vifaa hivyo uliratibiwa na Uwakilishi wa kitume na Patriaki wa Kilatino huko  Yerusalem na Caritas ya Yerusalem, tarehe 17 Juni 2020, kwa mujibu wa upatriaki huo. Aliyevipokea ni Padre  Gabriel Romanelli, Paroko wa parokia ya Familia Takatifu huko Gaza. Mchango huo ni sehemu ya juhudi zilizoanzishwa na Mfuko wa Dharura-covid-19, kwa utashi wa Papa Francisko, ili kusaidia nchi zilizoathirika zaidi na kuenea kwa virusi. Kati ya nchi hizi ni Siria, ambayo ilipokea mashine 10, na nyingine tatu zimepelekwa katika hospitali ya Mtakatifu Joseph kule Yerusalemu, wakati vifaa vya vya kupima Covid-19 vimepelekwa katika Hospitali ya Familia Takatifu ya Bethlehemu.

Ukosefu wa vipimo Gaza na vitanda

Zawadi ya Papa ni sehemu ya  upendo mkuu ambao Papa Francisko ameuonesha ukaribu wake: Fedha na hata  oksijeni kwa maeneo ambayo  ni magumu, halafu mashine za kupumulia na  vifaa vya matibabu, vifaa vya kiafya ambavyo vinasafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine ulimwengu kama vile hata  Ecuador, Romania,  Brazil, Uhispania, Napoli na Lecce, lakini pia hata kupiga simu kwa maaskofu, jumuiya , madaktari, wauguzi ambao wanapata mateso na ugumu, katika wadi za hospitali vile vile vyama vya kujitolea vilivyo mstari wa mbele. Kwa kila mmoja  Papa analo neno au ishara na shukrani nyingi kwao.Kulingana na kuenea kwa virusi huko Gaza mahali ambapo wanaishi karibu watu milioni 2 mamlaka ya kiafya mahalia wamelalamikia juu ya ukosefu wa vipimo na kuomba hata mashine  100 za kupumulia na vitanda 140 katika vyumba vya mahututi. Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Afya Palestina, huko Gaza, kesi 72 za virusi vya corona zimebainishwa tena na kufikia jumla ya kesi 1284 katika eneo la Kipalestina (takwimu za Juni 23).

Mashine moja ya upimaji wa virusi huko Gaza

Kufungwa kwa ukanda wa Gaza hata hivyo kumesaidia kutoeneza zaidi virusi japokuwa kesi zote ambazozipo zimetokana na watu waliotoka nje na ambao mara moja waliwekwa karantini. Vifaa vilivyotumwa na Papa vitasaidia kufanya utambuzi sahihi zaidi na mara tu watakapo vipeleka katika maabara ya Wizara ya Afya. Kiukweli kuna mashine moja tu huko Gaza ambayo inaweza kufanya ugunduzi, amesema Padre Gabriel Romanelli Paroko wa Gaza.

25 June 2020, 12:26