Tafuta

Vatican News
Ufunguzi tayari wa Majumba ya makumbusho Vatican kwa ajili ya wageni na tarehe 6 ufunguzi wa bustani ya Kipapa huko Castel Gandolfo Ufunguzi tayari wa Majumba ya makumbusho Vatican kwa ajili ya wageni na tarehe 6 ufunguzi wa bustani ya Kipapa huko Castel Gandolfo  (AFP or licensors)

Majumba ya makumbusho na bustani kiingilio ni bure kwa madaktari na wahudumu wa afya!

Kwa ajili ya kutoa shukrani kubwa kwa kile ambacho kimetendeka kwa moyo mkunjufu wakati wa kipindi cha dharura kwa madaktari wote,wauguzi, mafundina wahudumu katika vituo vya afya ya umma na binafsi nchini Italia wataweza kuingia bure kwa wiki nzima katika Majumba ya Makumbusho ikiwa ni pamoja na Bustani ya Kipapa huko Castel Gandolfo.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Majumba ya Makumbusho Vatican pamoja na Bustani za Kipapa vinapenda kuungana  na ulimwenguni kutoa hisia za shukrani kubwa na kwa moyo mkunjufu kwa wahudumu wote wa kiafya na wanafanyakazi wa sekta ya huduma ya afya kwa ishara iliyo rahisi sana, lakini iliyojaa maana na kusukumwa na imani kwamba sanaa na dawa vimeunganishwa na kusudi lililokubwa zaidi  yaani lile la  kumtunza mwanadamu kwa ukamilifu wake. Madaktari, wauguzi na wafanyakazi wote wa afya katika huduma kwenye vituo vya afya vya umma na vya kibinafsi katika eneo la Italia  kwa njia hiyo wataweza kutembelea bure maeneo haya ya urithi wa kiutamaduni na imani. Ili kuweza kuingia bure inatosha kujiwakilisha ukiwa na kadi ya kitambulisho kilichotolewa na maagizo ya wataalam au kampuni za huduma ya afya mahali pa kazi na kitambulisho ni mali yake. Promosheni pia imepanuliwa kwa rafiki msindikizaji.

Majumba ya makumbusho Vatican

Kwa mujibu wa taarifa kwa waandishi wa habari kutoka kwa Gavana wa serikali ya Vatican imetangazwa kuwa hatua hiyo itakuwa halali katika Majumba ya Makubusho Vatican kuanzia  Jumatatu tarehe 8 Juni hadi Jumamosi 13 Juni 2020 (Alhamisi tarehe 11 Juni 2020 Jumba la Makumbusho linafungwa). Wakati wa masaa ya ufunguzi yatakuwa kama ifuatavyo:Jumatatu hadi Alhamisi kuanzia saa 4.00 asubuhi masa ya Ulaya hadi  saa 2.00,usiku masaa ya Ulaya. Kuingia mwisho ni saa 12.00 jioni masaa ya Ulaya; na wakati, siku ya Ijumaa na Jumamosi kuingia ni kuanzia saa 4,00 asubuhi masaa ya Ulaya hadi saa 4 usiku masaa ya Ulaya; kuingia mwisho ni saa 2.00 usiku masaa ya Ulaya.

Bustani za Kipapa

Bustani za kipapa zitaweza kutambelewa na wageni kuanzia Jumamosi tarehe 6 Juni na Jumapili 7 Juni 2020 na baadaye Jumamosi 13 Juni na Dominika tarehe 14 Juni 2020. Jumba la Kitume la Castel Gandolfo na maajabu ya Bustani za huko Barberini zitatembelewa angalau kwa sasa na  wageni siku ya Jumamosi na Jumapili tu kuanzia saa 4 .00 asubuhi majira ya Ulaya hadi saa 12.00 jioni masaa ya Ulaya, kuingia kwa mwisho ni saa 11.00 jioni masaa ya Ulaya. Kwa ujumla eneo lote la Bustani na kwenye pembe za ziwa la Castel Gandolfo, vitafunguliwa tena milango yake tarehe 6 Juni 2020 baada ya kufungwa kwa kipindi hiki cha janga.

03 June 2020, 16:00