Tafuta

Vatican News
2020.06.11 harakati za Kanisa katika kutoa msaada katika kipindi hiki cha janga kwa watu wenye shida na maskini zaidi 2020.06.11 harakati za Kanisa katika kutoa msaada katika kipindi hiki cha janga kwa watu wenye shida na maskini zaidi 

Kard.Turkson:Baada ya janga umakini kwa waamini unahitajika!

Umefanyika mkutano tarehe 10 Juni 2020 wa Baraza la kipapa la huduma ya Maendeleo fungamani ya watu na vyombo vya habari Vatican.Mada msingi ilikuwa ni jinsi gani Kanisa mahali linajiandaa baada ya janga la virusi.Kardinali Turkson amesisitizia juu ya wachungaji wa Makanisa na wahudumu wao kuwa makini katika mahitaji ya jumuiya zao.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Kushirikishana habari haitoshi lakini pia hata kuandaa kwa njia ya mawazo ya pamoja ili kuweza kujenga kwa upya wakati endelevu baada ya janga la virusi.  Hii ni katika kutafuta ufunguo wa pamoja ambao unaweza kwa dhati kushirikishwa na ubinadamu wote hasa kuanzia na mapendekezo ya Papa Francisko ambaye amefafanua kila wakati kwamba kila kitu katika dunia hii kimesukana. Ni Lengo ambalo linatazamwa na Kanisa, Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya watu, (DSSUI) likiwa mstari wa mbele na Tume ya Vatican ya Covid-19, iliyoundwa kwa utashi wa Papa Francisko mwenyewe. Haya yote ndiyo yaliyozunguzwa kwa marefu na mapana katika mkutano wa tarehe 10 Juni 2020 wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya watu pamoja na vyombo vya habari Vatican. Wakuu wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo fungamani ya watu Kardinali Peter Turkson; Katibu wake Segundo Tejado Muñoz na Aloysius John, Katibu Mkuu wa Caritas Internationalis.

Mitazamo mitatu msingi

Janga ni tukio la kiulimwengu ambalo limekwisha haribu sana msimamo wa kimaitafa ambao  pia ulikuwa tayari ni mdhaifu, kwa kukuikumba hali halisi na sekta zote. Katika hali kama hii, Kanisa linahisi kwa dhati kujikita  katika kambi, hasa kwa utekelezaji wake kwenye mabara matano kwa njia ya matendo ya haraka ikwezekanao, yenye uwezo wa kufikia hali halisi zilizo maskini zaidi.  Misingi hiyo na matendo ya Caritas ambayo yanakuwa karibu na makanisa mahalia kwa ajili ya kuhamasisha na kukuza mipango ya misaada. Lengo la kwanza ni kurudisha hasa hadhi kwa kutoa chakula na vifaa vya kiafya , kama vile sabuni. Baadaye kuna mafunzo ambayo ni muhimu kwa namna ya kuzuia maambukizi zaidi ya virusi. Maono na ambayo ni kutazama na wakati huo huo kudumisha uhusiano wa nguvu ambao ni wa kidugu. Maana ya ushiriki wa umoja wa familia ya kibinadamu ni muhimu kwani unaruhusu jitihada za pamoja na zile za kibinafsi. Aidha Kardinali  Turkison awali ya yote ameonyesha uchungu  zaidi kwa familia nyingi ambazo zimepoteza wapendwa wao bila kuwapa mkono wa buriani na zaidi hasa kufanyiwa mazishi yasiyofaa. Kwa maana hiyo Kanisa linahitaji kuwa karibu na familia kama hizo amesititiza. “Ninawapa salam za rambi rambi wale ambao wamepoteza wapendwa ... Mazishi siku hizi  yanafanyika katika hali mbaya sana. Jamaa wengi hawana nafasi ya kuwa karibu na wapendwa wao hata wanapokufa na kuzikwa”amesema Kardinali.

Nyayo za Papa Benedikto XVI

Kardinali Turkison wakati wa kuhojiwa na Gazeti ‘Gudrun Sailer’ alisema kuwa muungano kati ya Papa Benedikto XVI na Papa Francisko,  ni mkubwa kwani Papa Mstaafu Benedikto XVI wakati wa hotuba yake kuhusu matumaini, anasema , “kuzungumza matumaini maana yake ni kuzungumza wakati ujao, na haiwezekani kuzungumza wakati ujao bila kuzungumza ya Mungu “ ambaye kwa hakika anapelekea kuzungumza na mwanadamu. Kwa maana hiyo ndiyo matendo ya Makanisa mahalia na matarajio ya Caritas katika mabara 5, katika mambo matatu makuu kuhusu hadhi, mafunzo na udugu.

Tume ya Vatican COVID-19

Tarehe 20 Machi 2020, Papa Francisko aliomba Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya watu kuunda Tume kwa ushirikiano na Mabaraza mengine ya kipa pa, na taasisi mbalimbali, ili kufafunua shauku na upendo wa Kanisa kwa familia nzima ya kibinadamu mbele ya janga la virusi vya corona au  COVID-19, na zaidi wakati wa kutathimini na kutafakari juu ya changamoto za kijamii , kiuchumi na kiutamaduni kwa nyakati zijazo na kutoa mapendekezo mapya ambayo yanakuwa kiongozi mkuu ili  kukabiliana nayo.

11 June 2020, 14:54