2020.06.19 Familia uhamishoni, LEV 2020.06.19 Familia uhamishoni, LEV 

Familia uhamishoni:Huduma kuhusu wahamiaji:tangu Papa Pio XII hadi Papa Francisko!

Katika siku ya Wakimbizi duniani kimetangazwa kitabu kipya kwenye duka la vitabu Vatican(LEV)ambacho kinapendekeza kwa upya usomaji wa Hati ya kitume ya Papa Pio XII,mawazo yake sanjari na ya Papa Francisko.Katika utangulizi wa kitabu hicho umetolewa na Andrea Riccardi na Padre Fabio Baggio.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Familia ya Nazareti iliyokwenda uhamishoni ya  Yesu, Maria na Yosefu ambayo ilikuwa ni  wahamiaji wa kwenda Misri na wakimbizi ambao walitoroka  hasira ya mfalme asiyemcha Mungu, ndiyo mfano na msaada wa wahamiaji wote na mahujaji wa kila kizazi kutoka nchi zote, wakimbizi wote wa hali yoyote  na ambao wakiongozwa na mateso au mahitaji wanalazimika kuhama nchi yao, jamaa na  wapendwa, majirani, marafiki wema, na kwenda nchi ya wageni. Haya yalikuwa ni maneno ya Papa Pio XII katika hati yake. Kunao mwaka 1953 Ulaya ilikuwa inapitia kipindi kigumu hasa cha athari za majanga ya Vita ya Pili ya Dunia na ilikuwa na wahamiaji wengi waliolundikana ndani. Inakadiriwa kwamba walikuwa ni wahamiajai milioni 60 wa Ulaya ambao walilazimika kuhama kwa sababu ya vita.

Ukaribu wa Kanisa kwa wakimbizi

Papa Pacelli, au Pio XII kwa kuonesha ukaribu wa Kanisa kwa wale ambao walilazimika kuhama kwa sababu ya mateso au mahitaji, ya kuhama alitangaza Hati ya kitume iitwayo Exsul Familia, yaani   familia uhamishoni Hati ambayo inanaki kuwa yenye thamani kubwa katika huduma ya nada hii ya wahamiaji, ambapo akikumbusha tangu mwanzo wa  maandishi yake kwamba wakristo wanaitwa kutazama uso angavu wa wakimbizi na waliolundikana ndani na wahamiaji ile  sura ya familia ya Nazarethi, sura ya mtoto mdogo Yesu na ya Marian a Yosefu.

Uwasilishaji wa jitihada za Kanisa

Maandishi ya lugha ya kiitaliano  ya Hati hiyo, ambayo inakumbukwa kidogo leo hii, haikuwa rahisi sana kupatikana. Kwa sababu hii, Byumba ya Uchapishaji wa vitabu Vatican imeamua kuchapisha kwa mara nyingine  tena sehemu ya kwanza na thabiti kabisa ya Hati ya Kitume, ambayo inataka  kuwasilisha na kuhamasisha jitihada za Kanisa kwa ajili ya wakimbizi na wahamiaji katika historia yake yote.

Familia uhamishoni

Kitabu hiki kilichopewa jina “ Familia katika uhamishoni" kinapatikana katika duka la vitabu Vatican (LEV) (chenye  kurasa 152 kwa bei yake  euri 10) ambacho kimetolewa utangulizi wake  ili kukisoma kwa unagalifu kikiwasilisha mwendelezo wa huduma ya kipapa  tangu Papa Pio XII hadi sasa  katika  muktadha wa kihistoria hii ya uhamiaji, kwa kuandaliwa na Padre  Fabio Baggio, katibu  msaidizi wa Kitengo cha  sehemu Wahamiaji na Wakimbizi cha Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya watu vile vile na mwanahistoria Andrea Riccardi ambaye pia ni mwanzilishi wa Jumuia ya Mtakatifu Egidio. Kwa kusoma kurasa hizi unaelewa zaidi juu ya mafundisho ya Papa Francisko kuhusu suala hili la sasa sambamba na kile kilichoandikwa na Papa Pius XII kwa wakati ule.

 

23 June 2020, 14:05