Tafuta

Baraza la Maaskofu Katoliki Ujerumani linawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kushikamana na Papa Mstaafu Benedikto XVI wakati huu anapomsindikiza Kaka yake katika ugonjwa! Baraza la Maaskofu Katoliki Ujerumani linawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kushikamana na Papa Mstaafu Benedikto XVI wakati huu anapomsindikiza Kaka yake katika ugonjwa! 

Mshikamano wa Sala na Papa Mstaafu Benedikto XVI.

Baraza la Maaskofu Katoliki Ujerumani linapenda kuchukua fursa hii, kumkaribisha kwa heshima, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI nchini Ujerumani. Itakumbukwa kwamba, hii ni mara ya kwanza kwa Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kusafiri kutoka nje ya Italia tangu alipong’atuka kutoka madarakani mwaka 2013. Mshikamano wa upendo na sala unahitajika katika kipindi hiki!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Askofu Georg Bätzing wa Jimbo Katoliki la Limburg, ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Ujerumani anasema, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI, amewasili nchini Ujerumani, tarehe 18 Juni 2020, ili kumtembelea kaka yake Monsinyo Georg Ratzinger ambaye kwa siku za hivi karibuni afya yake imeendelea kudhohofu sana kutokana na kuugua kwa muda mrefu pamoja na uzee! Kwa heshima na taadhima kubwa, Baraza la Maaskofu Katoliki Ujerumani linapenda kuchukua fursa hii, kumkaribisha kwa heshima, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI nchini Ujerumani. Itakumbukwa kwamba, hii ni mara ya kwanza kwa Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kusafiri kutoka nje ya Italia tangu alipong’atuka kutoka madarakani mwaka 2013.

Kwa miaka kadhaa, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI alikuwa ni Mwanachama wa Baraza la Maaskofu Katoliki Ujerumani, kabla ya kuteuliwa kushika nyadhifa mbali mbali katika maisha na utume wa Kanisa mjini Vatican. Inasikitisha kwamba, Baba Mtakatifu anawatembelea wakati huu, ambapo hali ya kaka yake mkubwa Monsinyo Georg Ratzinger, ambaye hali yake ni tete kutokana na magonjwa na uzee. Hata katika hali kama hii, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI amependa kuonesha uwepo wake wa karibu kwa kaka yake wa pekee! Baraza la Maaskofu Katoliki Ujerumani linapenda kuchukua fursa hii, kumhakikishia Papa Mstaafu Benedikto XVI uwepo wao wa karibu na kwamba, watamhakikishia maisha ya faragha wakati huu anapomuuguza kaka yake!

Ujerumani B16

 

 

20 June 2020, 07:29