Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Michael Kalu Ukpong, kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Umuahia, Nchini Nigeria. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Michael Kalu Ukpong, kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Umuahia, Nchini Nigeria.  (Vatican Media)

Mh. Pd. Michael Kalu Ukpong, Askofu Msaidizi, Umuahia, Nigeria!

Askofu mteule Michael Kalu Ukpong alizaliwa tarehe 15 Desemba 1964 huko Amaekpu Ohafia, Jimbo Katoliki la Umuahia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi ndani na nje ya Nigeria, tarehe 7 Agosti 1993 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Mwaka 2016 hadi mwaka 2018 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya “Coronata” huko Asaga Ohafia na Amekuwa pia Paroko!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Michael Kalu Ukpong wa Jimbo Katoliki la Umuahia, Nigeria, kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Umuahia. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule Michael Kalu Ukpong alikuwa ni Katibu mkuu wa Jimbo na Paroko wa Parokia ya “St. Theresa” Jimbo Katoliki la Umuahia. Itakumbukwa kwamba, Askofu mteule Michael Kalu Ukpong alizaliwa tarehe 15 Desemba 1964 huko Amaekpu Ohafia, Jimbo Katoliki la Umuahia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi ndani na nje ya Nigeria, tarehe 7 Agosti 1993 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Tangu wakati huo amewahi kuwa Paroko-usu. Katibu muhtasi wa Askofu, Paroko, Mhariri mkuu wa Gazeti la “Lumen Newspaper linalochapishwa na Jimbo Katoliki la Umuahia na hatimaye Paroko wa maisha ya kiroho huko Umudike kabla ya kwenda nchini Ujerumani kwa masomo ya juu kati ya mwaka 2004-2014 na kujipatia Shahada ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha “Regensburg”. Akiwa nchini Ujerumani aliendelea na utume wa Kipadre tangu mwaka 2013 hadi mwaka 2016. Mwaka 2016 hadi mwaka 2018 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya “Coronata” huko Asaga Ohafia. Tangu mwaka 2018 hadi kuteuliwa kwake alikuwa ni Katibu mkuu wa Jimbo la Paroko wa Parokia “St. Theresa” Jimbo Katoliki la Umuahia.

Papa: Uteuzi
01 June 2020, 10:55