Tafuta

Vatican News
Kitabu kiitwacho "Maisha baada ya Janga” kimetolewa katika Duka la Vitabu,Vatican (LEV.Ni mkusanyiko wa tafakari za Papa Francisko tangu tarehe 27 hadi 22 Aprili 2020. Kitabu kiitwacho "Maisha baada ya Janga” kimetolewa katika Duka la Vitabu,Vatican (LEV.Ni mkusanyiko wa tafakari za Papa Francisko tangu tarehe 27 hadi 22 Aprili 2020. 

VATICAN#coronavirus:“Maisha baada ya janga"ni mkusanyiko wa tafakari za Papa kipindi cha janga!

Tarehe 13 Mei 2020,Kitabu kilichopewa jina“Maisha baada ya Janga” kimetolewa katika Duka la Vitabu,Vatican (LEV)ambacho kinakusanya tafakari nyingi za Papa Francisko kuanzia tarehe 27 Machi hadi 22 Mei 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika kitabu kimoja kipya kwenye duka la vitabu Vatican, kimetolewa ambacho ni tunda la mkunyiko wa tafakari za Papa Francisko kuhusu dharura ya Covid-19, ambacho kimepewa jina la “Maisha baada ya janga”. Kitabu hiki pia kinapatika  katika muundo wa kidijitali na inaweza ukapakua bure.

Katika kitabu hiki kinakusanya tafakari za Papa Francisko alizotamka zikiwa katika maandishi na zile za kuzungumza kuhusiana na janga la virusi vya corona ambavyo vimesambaa katika familia ya binadamu duniani kote na kwa maana ya kuelekeza, kufariji na mwongozo wa kuanza kwa upya maisha ambayo yana ladha ya kuzaliwa kwa upya.

Hata hivyo hivyo ni safu ya vitabu nane kuanzia tarehe 27 Machi hadi tarehe 22 Aprili na ambavyo vinaweza kusomwa katika umoja wa mwendelezo wa wazo la Papa Francisko lenye utajiri wa ujumbe wa ubinadamu.

Utangulizi wa kitabu hicho umetiwa sahihi na  Kardinali Cardinale Michael Czerny, katibu wa kitengo cha wahamiaji na wakimbizi cha Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya kibinadamu. 

Katika kitabu hiki au hivyo nane Kardinali Czerny anaandika,kuwa vinaonesha njia yenye joto na ya umoja wa Papa Francisko, ambayo haipunguzi watu kwa vitengo vya kuhesabiwa, kipimo na kusimamiwa, lakini ni katik kuunganisha wote kwa ubinadamu wa pamoja na katika roho.

Pamoja na maono katika jitihada na matendo, Kardinali Czerny anahimitimisha akisema kuwa, Papa Francisko ameonyesha jinsi gani  sala ni msingi kwa ajili ya kuelekeza  mtazamo wa macho yetu katika tumaini na zaidi jinsi sala ikipunguzwa kuna hatari ya kutelekezwa. Vitabu hivyo vinaweza kupakuliwa kupitia Tovuti ya Duka la Vitabu Vatican (LEV). Tovuti ya Duka la Vitabu:https://www.vaticannews.va/it/lev.html.

 

14 May 2020, 15:43