Tafuta

Vatican News
Wosia wa  “Ut unum sint” wa Mtakatifu Yohane Paulo II  kuhusu uekemene uliotiwa sahini tarehe 25 Mei 1995, Wosia wa “Ut unum sint” wa Mtakatifu Yohane Paulo II kuhusu uekemene uliotiwa sahini tarehe 25 Mei 1995,  

Ni miaka 25 ya “Ut unum sint", kati ya unabii na upinzani

Wito kwa Wakristo wote ili waweze kujibu maombi ya Yesu kwa ajili ya umoja wa wanafuasi wake.Wosia wa Papa Wojtyla unasaidia kutazama hali halisi ya Jumuiya za Wakristo leo hii na kupyaisha jitihada za kiekumene.

Na Sergio Centofanti

Baada ya miaka ishirini na tano ya Wosia wa  “Ut unum sint” wa Mtakatifu Yohane Paulo II  kuhusu uekumene uliotiwa sahini tarehe 25 Mei 1995, bado unahifadhi ule uhai na nguvu yake ya kibanabii. Kwa mtazamo wa haraka unaelekeza hatma ambayo utafikiri ni iko mbali, yaani ya umoja wa kikristo. Yesu mwenyewe anataka  na kabla ya kukabiliana na Mateso alisali kwa Baba yake  ili walio wake wawe na umoja.

Papa katika umoja

Papa Wojtyla alihisi kwa nguvu shauku kubwa ya Bwana na akaifanya kuwa kama ya kwake na uekuemene ukawa ndiyo moja ya vipaumbele vya Kipapa, kwa sababu migawanyiko ya kikristo ni kashfa inayoshambulia kazi yenyewe, hivyo anaandika kwamba “kuamini katika Kristo maana yake ni kupendelea umoja”. Ni tendo la utii ambalo hupanua upeo wa moyo na akili.  Hata hivyo Papa mwenyewe mwenye kupenda umoja alikumbana na uchungu mkubwa kwa upande wa waasi wa Mungu, anaposema kuwa “kuna ndugu wengine ambao haelewi mwamko wa siku za mbele”.  Hati yake hiyo ilikuja miaka 7 mara baada ya hutoaji wa daraja la uaskofu bila idhini ya Papa kunako tarehe 30 Juni 1988 na Askofu Mkuu Marcel Lefebvre., ambaye alikataa baadhi ya masasisho na maamuzi ya Mtaguso wa  II wa Vatican.

Yohane Paul II alishutumiwa

Askofu huyo wa utamaduni wa Ufaransa anamshtumu Papa wa Kipoland  na Mtaguso wa II wa Vatican  kwa kile alichoita “uekemene wa uwongo” ambao anasmea unaharibu imani ya kweli na kupelekea “Kanisa kuharibiwa na Wakatoliki  kuasi imani yao”. Yeye alikuwa na wazo kuwa Mungu amemkabidhi utume wa kupinga “Roma ya sasa, iliyoambukizwa na mitindo ya kisasa kwa sababu iweze kuwa tena Roma Katoliki na kurejesha milenia zake mbili za utamaduni”. Kwa maoni yake ni kwanza walianzisha wazo la waprotestanti katika Misa na sakramenti. Lefebvre alifariki kunako mwaka1991.

Wafuasi wake wanautazama Wosia wa Yohane Paulo II kwa sababu, na wanadai  kuwa siyo tu unaongoza katika uhusiano wa mafunzo, lakini pia kiukweli tayari unao. Nafasi ambayo ina wazo lisilokamilika na linalokinzana la tamaduni, kwa mujibu wa Papa Wojtyla katika Barua ya Kitume ya “Ecclesia Dei”, haijakamilika, kwa sababu halizingatii kuwa Tamaduni ni hai na inakua kwa vile inarithisha kutoka kizazi hadi kizazi, bila kuwekwa tarehe ya kihistoria iliyoanzishwa. Upinzani ni kwa sababu Utamaduni hauwezi kutenganishwa na umoja na Papa na wachungaji ulimwenguni kote

Majadiliano ni kipaumbele kinachoruhusu ugunduzi usiotarajiwa

Katika hati ya kipapa inatazama mbele kwa ujasiri, inaelekeza majadiliano kama kipaumbele na ni njia ya lazima ya kugundua utajiri wa wengine. Inatazama hatua muhimu zilizofanyika kuelekea umoja na makanisa mengine na jumuiya ya kikristo kuanza na  kuondoa vikwazo vya kutengwa kati ya Roma na  Constantinople na kutoka katika Tamko la Kikristo la pamoja na Makanisa ya zamani ya Mashariki. Ni njia ambayo inaruhusu uvumbuzi usiyotarajiwa katika ufahamu kwamba “utofauti halali haupingi umoja hata kidogo.” Mabishano na maneno yasiyoweza kuvumiliwa katika hati hiyo  yamebadilika kuwa taarifa zisizokubaliana ambazo kiukweli matokeo ya mitazamo miwili ililenga kukagua ukweli huo huo, lakini kutoka katika pembe mbili tofauti”. Ni njia ambayo inasaidia “kugundua utajiri wa ukweli usioelezeka” na uwepo wa mambo ya utakaso “zaidi ya mipaka inayoonekana ya Kanisa Katoliki”.

Ufafanuzi wa ukweli unaweza kuwa mwingi

Sio suala la kurekebisha amana ya imani” na ya kubadilisha maana ya mafundisho ya Kanisa, anafafanua  Papa Wojtyla, lakini ni kielelezo cha ukweli unaoweza kuwa wa aina nyingi kwa sababu mafundisho lazima yawasilishwe kwa njia ambayo inaeleweka kwa wale ambao Mungu mwenyewe amewatayarisha  kwa kila tamaduni yoyote ile, kuepuka aina yoyote ya “ubaguzi au ubaguzi wa rangi au upendeleo”, kama vile majivuno ya utaifa.

Mazungumzo ya mafundisho kufikia mazungumzo ya upendo

Wosia huo unelekeza ulazima ambao uwe mtindo wa utangazaji  imani katoliki na ambao inatakiwa  kwamba usiwe kizingiti cha mazungumzo na ndugu, katika utambuzi ambao ni uongozi katika ukweli wa mafundisho Katoliki. Kanisa, anasema Papa Yohane  Paul II, limeitwa na Kristo katika mageuzi haya ya kuendelea” na ambayo yanaweza kuhitaji marekebisho ya uthibitisho na mitazamo. Majadiliano, anakumbuka hayajikiti katika kuzungukia mafundisho peke yake, lakini pia kuhusisha mtu kwa sababu pia ni mazungumzo ya upendo”. Ni kwanjia ya upendo kwamba inazaliwa shauku ya umoja. Ni mchakato wa safari inayohitaji kazi ya uvumilivu na ujasiri. Kwa kufanya hivyo, ni ulazima wa kuwa na  majukumu”

Ukuu wa maombi:kuomba yaliyo muhimu

Katika uekumene, Papa Yohane Paulo II anabainisha juu ya jukumu la sala ya pamoja. Wakristo, wakiomba pamoja, hugundua kuwa kile kinacho waunganisha ni nguvu zaidi kuliko kile kinacho watengenisha. Mabadiliko ya  Kiliturujia yaliyofanywa na Kanisa Katoliki na Jumuiya nyingine za kidini yameruhusu ubadilishaji juu ya mambo  muhimu na kwa pamoja, na zaidi, tunageukia  Baba kwa moyo mmoja. Wakati mwingine anasema Papa Yohane Paulo II kuwa uwezo wa kufikia hatimaye umoja halisi hata kama aujawa kamili lakini unaonekana kuwa karibu zaidi. Nani angeweza kufikiria katika karne iliyopita?

Jitihada za pamoja kwa ajili ya uhuru, haki, amani

Kati ya hatua za mbele kwenye mchakato wa njia ya uekuemen, Wosia unaonyesha ukuaji wa  kushirikiana kwa Wakristo katika dhehebu mbali mbali za kikirto mbele ya jitihada  kwa ajili ya uhuru, haki, amani, mustakabali wa ulimwengu: sauti ya pamoja  ya Wakristo ina nguvu  zaidi kuliko sauti ya pekee kuwa na ushindi wa haki na mahitaji ya wote, hasa maskini, wanyonge na wasio na ulinzi”. Kwa Wakristo ,  Papa Wojtyla anasisitiza, siyo suala la vitendo vya kibinadamu tu, bali la ni kujibu neno la Yesu, kama tunavyosoma katika sura ya 25 ya Injili ya Mathayo: “Nilikuwa na njaa na ulinipa chakula ...”.

Kadilisha lugha:kutoka katika hukumu hadi msamaha wa pande zote

Papa Yohane Paulo II anatoa wito wa kuwa na mabadiliko ya lugha na mitazamo: ni lazima kuepuka mtindo wa fujo na wa kupinga, ushindani ambao huonesha kila kitu ni hasi, tabia ya kujifungia hivyo siyo ya Kiinjili katika kuhukumu wengine na kudharau ambayo inayotokana na dhana mbaya. Badala yake, lazima tufanye kila linalowezekana, kwa msaada wa Mungu, kubomoa kuta za migawanyiko na kutoaminiana, kushinda vizuizi na ubaguzi, kuondoa maneno maneno ambayo yanaumiza, kuchagua njia ya unyenyekevu, upole na ukarimu wa kindugu. Kwa hivyo, baada ya muda hatasikia mazungumzo tena juu ya wazushi au maadui wa imani, lakini juu ya Wakristo wengine, wabatizwa wengine. Upanuzi huu wa kitabu, anasisitiza Papa Wojtyla, hutafsiri mabadiliko ya kushangaza ya fikra”. Ni njia ya uongofu ambayo hupita katika njia ya lazima ambayo ni toba ya pamoja kutumbu kwa makosa yaliyofanywa. Na Papa Yohane Paulo II anaomba msamaha wa dhambi zilizofanywa na wajumbe wa Kanisa.

Ukuu wa Papa:huduma ya upendo

Umoja kamili una kielelezo kinachoonekana cha Petro na Papa Yohane Paulo II anatoa wito kwa Jumuiya zote za Kikristo il kupata mtindo wa zoezi la ukuu wa Petro ambalo, licha ya kukataa njia yoyote muhimu ya utume wake inajifungulia katika hali mpya kama huduma ya upendo inayotambuliwa na mmoja na mwingine.

Kanisa katika njia kuelekea umoja

Ut unum sint ni ufupisho wa unaongaza katika safari ya Kanisa kupitia miaka yake 2000 ya historia. Ni taa inayoonyesha njia tuliyomo kwa kufuata ule mwelekeo sawa na wale waliotutangulia. Inaonyesha tabia hai ya Tamaduni, ambayo kama “Dei Verbum” asemavyo kuwa inatoka katika asili ya Mitume na inaendelea katika Kanisa chini ya msaada wa Roho Mtakatifu. Na shukrani kwa Roho, akili ya imani inakua. Katika safari hii anasema Papa Yohane Paulo II akimnukuu Mtakatifu Cyprian ndugu lazima wajifunze kwenda kupatanishwa altareni, kwa sababu Mungu hakubali dhabihu ya wale wasiopatanishwa”. Badala yake, dhabihu kubwa zaidi ya kumtolea Mungu ni amani yetu na maelewano ya kidugu. Ni watu waliokusanyika katika umoja wa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Huu ni mwaliko wa mwisho wa Papa Wojtyla: akiomba Bwana kwa neema hiyo ya kututayarisha sote katika dhabihu ya umoja.

25 May 2020, 14:03