Tafuta

Vatican News
2020.05.30 Maktaba ya Kitume Vatican  2020.05.30 Maktaba ya Kitume Vatican  

Tarehe Mosi Juni kufunguliwa Maktaba na Hifadhi za Nyaraka za Kitume!

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Vatican zinabainisha kuwa tarehe Mosi Juni 2020,Maktaba na Hifadhi za Nyaraka za Kitume vinafunguliwa kwa wataalam na watafiti,mara baada ya miezi kadhaa ya kufungwa kutokana na janga la kidunia la kiafya.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baada ya kipindi cha kufungwa shughuli mbali mbali za Vatican kama ilivyo katika ulimwengu wote kutokana na janga la kidunia la kiafya, Maktaba na Pango la Hifadhi ya Nyaraka za Kitume Vatican, vitafunguliwa tena. Kumbu kumbu ni ya umoja ambayo ina msingi kwa ajili ya dini kibiblia. Ekaristi na sakramenti mahali ambamo panabubujika Kanisa ni maadhimisho ya kumbu kumbu ya zawadi binafsi ya ubinadamu kuanzia na Yesu: "Huu ni mwili wangu uliotolewa kwa ajili yetu, fanyeni kwa kunikumbuka Mimi" (Luka 22, 19). Sikiliza Israeli, ni sala msingi wa kiliturujia ya kiyahudi ambayo inawakilisha kumbu kumbu kama hali msingi wa utakatifu "ili mpate kukumbuka na kuyafanya maagizo yangu yote, na kuwa watakatifu kwa Mungu wenu" (Hesabu 15, 40).

Kwa njia hiyo kukumbuka ni amri ya wokovu kwa ajili ya wayahudi na wakristo kwa kupitia katika kufungua na kujiweka katika usikivu (Shemà Israeli: yaani "sikiliza israeli" ambayo hutenganisha mtu kutoka kwake binafsi dhidi ya udanganyifu mbaya kwa kuzingatia uzoefu wake kwa ujumla, kama ukweli kamili, ambao unadhibitisha hali ya mwanadamu kwa kiwango cha kutosha na cha kipekee, ambacho hakiachi nafasi ya mwingine, kwa wengine na mengine. Na ndiyo moja ya misingi ya utafiti katika nyaraka kwenye pango la hifadhi za kitume Vatican, licha ya mambo mengi ya kihistoria, na kiutamaduni wa utume wa mapapa na na historia ya maisha ya mwanadamu kwa ujumla. 

30 May 2020, 08:51