Mwaliko wa kufunga na kusali katika siku ya sala tarehe 14 Mei 2020 Mwaliko wa kufunga na kusali katika siku ya sala tarehe 14 Mei 2020  

Tarehe 14 Mei sala,kufunga na tafakari kwa wote!

Ni masaa machache kabla ya siku ya sala,ya kufunga na kuomba kwa ajili ya ubinadamu wote tukio linalotazamiwa tarehe 14 Mei kwa mujibu wa Kamati Kuu ya Udugu wa kibinadamu.Wazo kuu la Cenap Aydin,Mwanzilishi na mkurugenzi wa Taasisi ya Tevere kwa ajili ya Majadiliano ya kidini na Mafunzo ya Kiislam anasema ni wakati sasa wa kusali kwa pamoja.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika wakati huu wa shida, iliyosababishwa na janga la Covid-19, zaidi ya michakato ya kila mmoja anayofanya ili kujilinda na virusi, imafikia wakati hata wa kujikita katika sala ili kutafakari kwa kina. Ni kwa mujibu wa  Cenap Aydin Mwanzilishi na mkurugenzi wa Taasisi ya Tevere kwa ajili ya Majadiliano ya kidini na Mafunzo ya Kiislam mjini Roma. Katika siku ya tarehe 14 Mei iliyowekwa ya sala, kufunga na kumwomba Mungu kwa ajili ya ubinadamu ulioshambuliwa na janga na ambao ni siku iliyopendekezwa na  Kamati Kuu ya Udugu wa kibinadamu inayoundwa na viongozi wakuu wa kidini ili kumuunga mkono Papa Francisko. Hawa wameongozwa kwa Hati ya Udugu wa Kibinadamu wa kuishi pamoja iliyotiwa sahini huko Abu Dhabi kwa upande wa Papa Francisko na Imam Mkuu wa al-Azhar, Dk. Al Tayyeb. Kamati hiyo imependekeza kumwomba Mungu kwa sauti moja ili aweze kulinda ubinadamu huu, na kuweza kuusadia ushinde janga hili.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo Aydin anasema siku hiyo ya tarehe 14 Mei kwa hakika haigusi watu wenye imani tu, lakini kwa binadamu wote. Mpango wa Papa Francisko, ni mpango ambao unawaunganisha wote. Yeye kila wakati anawaomba waamini na wasio waamini kusali hasa kwa ajili ya amani, na zaidi anawaomba watu wote kuwa na shauku ya amani,  ya ustawi, na  kwa ajili ya wema wa wote na ndiyo mwaliko ambao unagusa wote. Kadhalika mkurugenzi huyo amesema, Siku ya terehe 14 Mei inaangukia katikati ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, mwezi wa kufunga kwa waislamu na suala la  kufunga kwa namna hiyo litawatazama watu wote na siyo kwa mara ya kwanza , anathibitisha, kwani anakumbuka kuwa ni sawa sala na mwaliko wa kufunga ulioombwa na Mtakatifu Yohane Paulo II alipokuwa akiomba amani kwa ajili ya nchi ya Bosnia kutokana na vita vilivyotokea kati ya mwaka 1993 na 1994.

Aidha Aydin amekumbuka na kutaja wakati wa sala ya Malaika wa Bwana kunako tarehe  18 Novemba 2001, wakati Mtakatifu Yohane Paulo II alipowaalika siku moja ya kufunga na kusali kufuatia na majanga ya kushambuliwa  kwa majengo mjini New York na Washington DC, kunako tarehe 11 Septemba 2001, hata wakati  huo ilikuwa ni kipindi cha mfungo wa Ramadhani, ambapo aliwaalika waislamu na wakatoliki kutenga siku ya kufunga na kusali kwa pamoja.

Mkurugenzi Cenap pia katika kutazama sura ya Maria kwenye maandiko ya Kiislamu yaani katika Qur'an Tukufu anasema yapo mambo mengi ambayo yanafanana na familia ya kibinadamu, na kwa namna ya pekee jambo moja la mateso, ambayo hayabagui, hayatazami utaifa, dini na wala kabila. Habari mbaya sana za kipindi hiki, zinatufanya tukaribiane mmoja na mwingine na kutufanya tuunganishe nguvu ambazo zinaweza kuleta suluhisho la haraka. Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo katika wazo la Mama wa historia kwenye mwezi wa Maria anasema, “katika Qur’an  sura ya 9 Maria yaani ‘Maryam’, alialikwa na Mungu kwa mujibu wa utamaduni wa Kiislamu, kudumisha mfungo kwa namna ya pekee neno la kubaki kimya wakati Yesu anazaliwa”. “Maria alikuwa na wasiwasi sana juu ya jinsi ya kujibu watu wake, na kwa hivyo tunaona Mariamu, ambaye hayazungumzi, anakaa kimya, kwa kufunga, huku akiomba, akitafakari akisubiri majibu kutoka kwa Mungu. Leo, katika hali nyingine, tunaweza kuliona tukio hili katika Qur’an. Tumegundua udhaifu wetu tena, tumegundua kuwa sisi ni wadhaifu sana, lakini sasa ni udhaifu huo inaotusukuma kuunganika tena katika sala, kufunga, katika upendo unaotukumbatia na kwa njia ya maombi katika upendo wa Mungu " 

12 May 2020, 15:00