Tafuta

Vatican News
2020.05.26 Padre Hans Zollner mhusika wa Tume ya maandalizi ya Mkutano wa Ulinzi wa Watoto katika Kanisa 2020.05.26 Padre Hans Zollner mhusika wa Tume ya maandalizi ya Mkutano wa Ulinzi wa Watoto katika Kanisa 

Mei 29 itafanyika semina kupitia mtandao juu ya ulinzi wa watoto!

Semina wa njia ya mtandao kwa madhumuni ya kuruhusu wataalam wa usalama kushirikishana mazoea mazuri na zaidi katika hali za sasa na ile ya kawaida.Mkutano wa Kimataifa wa ulinzi unaohusika na mafunzo kwa wale wanaohusika katika ulinzi wa watoto utashirikishana na wataalam mbali mbali kwenye sekta hiyo ili kutoa mjadala.Mkutano wa kwanza utafanyika tarehe 29 Mei 2020.

Mkutano wa Kimataifa wa Ulinzi na Usalama  wa watoto (ISC), ambao kila mwaka hukusanya pamoja wawakilishi wa Kanisa, wataalamu na zaidi wataalam wa kisayansi juu ya mada ya ulinzi wa watoto ili kushirikishana maarifa na mazozi bora, umeandaa mfululizo  mpya wa semina  kupitia mtandaoni kuanzia tarehe 29 Mei 2020 ili kuweza kujadiliana pamoja, kwa kuongozwa na kauli mbiu Kanisa salama zaidi. Mfululizo wa semina hizo utazingatia njia ambazo wataalam wa kulinda wanajibu jumuiya, hasa kwa waathirika kwa kuimarisha mazoea mazuri ambayo tayari yamekomaa na inakusudia kuhamasisha Kanisa Katoliki na mashirika mengine ya kidini katika kutekeleza mipango yao ya ulinzi licha ya shida kubwa inayotarajiwa kufuatia na janga la Covid-19.

Wasiwasi kuhusu ulinzi wa watoto kufuatia na janga la uchumi

Kwa mujibu wa Padre  Hans Zollner, Mhusika wa Kamati ya maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa  wa ulinzi na Usalama  wa watoto (ISC), amebainisha kuwa kwa hakika kuna wasiwasi, kuhusu kupunguzwa kwa mipango ya kulinda watoto na watu wazima wanaoishi katika mazingira magumu, kufuatia mzozo na ugumu wa uchumi wa sasa. Kwa maana hiyo ameongeza kusema,  “Hatuwezi kuruhusu uwekezaji wetu katika usalama wa watoto kwa njia sawa na shughuli zozote za kijamii na za kielimu”.

Kipeo cha kiafya na kipeo cha haki za watoto

Takwimu zilizoripotiwa na vyombo vya habari, katika nyakati za janga, zinaonyesha kuongezeka kwa ukatili dhidi ya watoto na kuongezeka kwa visa vya ukatili wa majumbani katika wiki za hivi karibuni. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema kuwa shida ya kiafya iliyosababishwa na Covid-19 inageuka haraka kuwa shida ya haki za watoto, na wataalam wa lango la Ulinzi wa watoto wameelezea mashaka na wasiwasi juu ya watoto katika majumba hayo mbayo yangetakiwa kuwa mahali pa salama kwa ajili ya wote.

Mkutano wa kwanza kwa njia ya mtandao utafanyika tarehe 29 Mei 2020 saa 9:00 alasiri, ambapo kama walivyofahamisha Tume ya maandalizi ya mkutano kuhusu  Ulinzi wa watoto, Kanisa ndiyo linachukua majukumu ya kulinda wakati wa kipindi hiki cha janga na kutilia maanani kwa namna ya kulinda waathiriwa.

26 May 2020, 17:28