Tafuta

Vatican News
Kuanzia trehe 31 Mei 2020,Papa anarudi katika dirisha lake la kawaida kusali sala ya Malkia wa Mbingu. Kuanzia trehe 31 Mei 2020,Papa anarudi katika dirisha lake la kawaida kusali sala ya Malkia wa Mbingu.  (Vatican Media)

Pentekoste:Sala ya Malkia wa Mbingu katika uwanja wa Mtakatifu Petro!

Tarehe 31 Mei 2020 ambapo Mama Kanisa anaadhimisha Sikukuu ya Ujio wa Roho Mtakatifu,Papa Francisko ataadhimisha Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro bila waamini na katika dirisha la ofisi yake atasali sala ya Malkia wa Mbingu kwa uwepo wa waamini katika uwanja wa Mtakatifu Petro utakao kuwa umelindwa na vikosi vya usalama,kuhakikisha usalama unaotakiwa.

VATICAN

Kwa mujibu wa msemaji mkuu wa Vyombo vya Habari Vatican kuhusu maadhimisho ya sherehe za Ujio wa Roho Mtakatifu (Pentekoste) tarehe 31 Mei 2020, ni kuwa  saa 4.00 asubuhi, majira  ya Ulaya, maadhimisho ya misa hiyo itakuwa mubashara bila waamini katika kikanisa cha Sakramenti Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Mara baada ya misa hiyo, saa 6.00  kamili Papa Francisko kwa mara nyingine tena ataanza sala ya Malkia wa Mbingu kwa waamini watakao kuwa wamekusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, mahali ambapo vikosi vya ulinzi na usalama, watahakikisha usalama wao hata kuwaongoza waamini wafuate kanuni za lazima kujilinda na kuwalinda wengine.

Ikumbukwe kuwa ilikuwa mnamo tarehe 8 Machi 2020 ambapo Papa Francisko kwa kufuata sheria ya kuzuia mikusanyiko na kutokana na kuenea kwa janga la virusi vya corona au covid-19, alikuwa amehamia ndani ya Maktaba ya Jumba la Kitume ili kusali wakati wa sala ya Malaika wa Bwana na kama ilivyo fuata hata katesi za kila Jumatano.

Siku ile Papa Francisko alisema kuwa Sala ile ilikuwa kidogo ya kushangaza kwamba alihisi kuwa kama amefungiwa ndani ya maktaba lakini kwamba alikuwa lakini anawaona na kuwa karibu nao. Tangu wakati huo kwa hakika kamera zimeweza kumwonyesha mara nyingi, kwa mfano baada ya sala za Dominika akichungulia dirishani, ili kubariki au kiwanja kikiwa wazi bila mtu au waamini wachache ambao polepole walirudi kumsalimia kwa mbali.

26 May 2020, 16:36