Tafuta

Vatican News
Ni kwa njia ya kuwa pamoja tu hasa katika kubeba majukumu ya walio wadhaifu zaidi inawezakana kushinda changamoto za ulimwengu. Ni kwa njia ya kuwa pamoja tu hasa katika kubeba majukumu ya walio wadhaifu zaidi inawezakana kushinda changamoto za ulimwengu. 

Kusheherekea Kipindi cha Uumbaji pamoja na familia ya kiekumene!

Katika matazamio ya kilele cha Siku ya Kuombea Utunzaji Bora wa Mazingira,Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya binadamu imeandika barua kwa kutoa mwaliko wa kuhamasisha jitihada katika Mwaka Maalum wa Laudoto sì ili kujibu kilio cha Dunia na kilio cha maskini.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika barua iliyotiwa sahini na Askofu Bruno-Marie Duffé, Katibu wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya binadam inasema kuwa “Tuwahimize watu wa Mungu kuharakisha hatua zao katika kuelekea njia mpya za Kanisa,  kwa ajili ya ekolojia fungamani na mipango ya shughuli za Kipindi cha Uumbaji. Ameandika barua hiyo akiwashauri kusheherekea pamoja na familia ya kiekumene katika kipindi kinachoanzia tarehe 1 Septemba, sambamba na Siku ya Kuombea Utunzaji Bora wa Mazingira hadi tarehe 4 Oktoba, katika siku kuu ya Mtakatifu Francis wa Assisi.

Kujibu kulio cha dunia

Mwisho wa Wiki ya Laudato Si na baada ya kuanza kwa Mwaka maalum wa Maadhimisho ya Wosia wa Papa Francisko, uliotangazwa miaka 5 iliyopita, Baraza hili linakumbuka kuwa Kipindi cha Uumbaji ni kwa mujibu wa kile alichosema Papa kunako 2019 ya kwamba, “ni kipindi cha kusali kwa kina na hatua za dhati kwa faida ya nyumba yetu ya pamoja na kuwa na mazoea ya kutafakari maisha yetu, kuchukua hatua  za kinabii, na  kwa kufanya hata uchaguzi wa ujasiri”. Kwa maana hiyo Baraza hili linasisitiza kuwa ni mwaliko wa kujikita katika kambi kwa kufuata mwongozo wa Wosia wa Kitume wa Querida Amazonia. Na hii wanasahuri ni katika kuanzisha mipango kama misa maalum au Hija kwa miguu, kufanya mazoea endelevu au uhamasishaji wa kujibu kilio cha dunia kama ilivyo hata kilio cha masikini, ili kuweza kutekelezwa wakati huu maalum.

Walinzi wa kazi ya Mungu

Kwa kunukuu maneno ya Papa Francisko, barua hii inethibitisha kuwa “Jibu la lazima na la dharura hasa katika nyakati za janga ambalo linatuonyesha kwamba ni kwa njia ya upamoja tu hasa katika kubeba majukumu ya walio wadhaifu zaidi, inawezakana kushinda changamoto za ulimwengu”. Katika ukosefu wa uhakika na majaribu kwa ajili ya walio hatarini, zaidi inafanya kutambua kuwa kila kitu kimeunganishwa na kwamba ni muhimu kujenga tena mahusiano ambayo tumevunja. Tunatambua kuwa lazima tukue zaidi na zaidi katika mshikamano na tusaidiane mmoja na mwingine kidugu.

Maaskofu na taasisi za kidini zihimize kusaidia watu wawe na utambuzi

Katika barua ya Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya watu, inawatia moyo maaskofu na taasisi za Kanisa ili zihimize kuwasaidia waamini waweze kuwa na utambuzi  wa kuishi jukumu kwa maana ya kuishi wito kama  walinzi wa kazi ya Mungu ni sehemu muhimu ya uwepo wa fadhila na siyo kufanya kitu cha  cha hiari na hata sio mantiki ya pili ya uzoefu wa Kikristo (rej. Laudato si '217). Ni kipindi cha kuzaliwa upya na kupyaishwa uhusiano na dunia.

Jitihada za Baraza la kipapa la Huduma ya maendeleo fungamani ya watu

Kwa sasa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo fungamani ya watu, inaendeleza jitihada za kazi ya kushirikisna na kutoa jibu la ulimwengu wakati huu wa janga la kidunia, kukabilisna iwe katika mahitaji ya haraka kwa wale wanaoteseka wakati huu, au iwe mahitaji , kwa kipindi kirefu ili kujenga jamii ili ya haki zaidi. Kwa maelezo zidi kuhusu “Kipindi cha  mantendo ya Uumbaji, kilichotayarishwa na Tume tendaji ya uekumene, unaweza kufungua katika Tovuti iliyoundwa: https://seasonofcreation.org/it/home-it/

25 May 2020, 14:50