Tafuta

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataaifa azungumza na Vatican Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataaifa azungumza na Vatican  

Katibu Mkuu Guterres:Tishio la ulimwengu linahitaji mshikamano

Gazeti la Osservatore Romano limetangaza mahojiano ya aina yake na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na vyombo vya habari Vatican.Katika maeneno yake anaoutambuzi wa kina kwa Papa Francisko kuunga mkono na katika kuendelea kutoa wito wa kusitisha vita vya kidunia.Katika mahojiano hayo anabainisha migorogoro ya janga la covid-19,silaha,haki za binadamu husani nyanyaso za wanawake na wasichana na uchafuzi wa mazingira.Inahitajika mshikamano wa umoja na upyaisho wa ulimwengu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika mahojiano na Mkurugenzi wa Gazeti la Osservatore Romano, Vatican, Dk. Andrea Monda na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bwana Antonio Guterres, amethibitisha ni kwa jinsi gani janga la virusi vya corona ni kengele ya hatari. Tishio la dunia la vifo, linahitaji umoja mpya na mshikamano. Katibu mkuu akijibu swali la  wito wake wa  hivi karibuni kwa ajili ya amani katika dunia iliyo shambuliwa na janga, ameanza kwa kumshukuru kwa kina Papa Francisko  kwa utambuzi na kuunga mkono kuhusu wito wake wa ulimwengu wa kusitisha vita na kazi ya Umoja wa Mataifa. Yeye anasema kwa jitihada zake, Papa, shauku zake na miito yake mbalimbali kuhusu umoja na mshikamano , vinathibitisha thamani msingi ambazo zinaongoza kazi yao katika kupunguza mateso ya kibinadamu na kuhamasisha hadhi ya binadamu.

Alipotoa wito wake kuhusu kusitishwa kwa vita amesema kuwa, ujumbe wake ulikuwa rahisi kwa sehemu husika za migogoro duniani kote, kwani mapigano lazima yaishe  kwa namna ya kuweza kujikita na mapambano ya adui wa pamoja Covid-19! Aidha amesema kuwa hadi sasa,ameungwa mkono na nchi 115, za serikali na  kanda na zaidi ya makundi 200 ya kijamii, yakiwemo hata viongozi wa kidini. Makundi 16 yanayotumia silaha wameanza kuacha vurugu. Na zaidi watu milioni moja wametia sahihi kupitia mtandao katika kuunga mkono suala hili.  Hata hivyo amebainisha kuwa  kutoaminiana kunaendelea kuwa mkubwa, na ni ngumu kutafsiri ahadi hizi kuwa hatua ambazo zitafanya mabadiliko katika maisha ya wale ambao wanakabiliwa na athari za mizozo.

Bwana Guterres vile vile ameongeza kusema kuwa  wawakilishi wake na wajumbe maalum wanafanya kazi bila kuchoka ulimwenguni kote, na ushiriki wake wa  moja kwa moja inapohitajika, kwa  kubadilisha nia yake kwa ajili ya kitisha mapigano. Kadhalika amethibitisha  ni kwa njia gani anaendelea kuwasihi wahusika katika mzozo, na wale wote ambao wanaweza kuwashawishi, kuweka afya na usalama wa watu kwanza.

“Napenda pia kukumbusha wito mwingine ambao niliutoa na ambao  ninafikiria ni muhimu ni wito wa amani ya nyumbani. Ulimwenguni kote, pamoja na kuenea kwa janga hili, tunashuhudia pia kuongezeka kwa dhuluma dhidi ya wanawake na wasichana”. Nimeomba serikali, asasi za kiraia na wale wote wanaoweza kusaidia ulimwenguni kuhamasisha ili kuwalinda wanawake. Pia nimeomba viongozi wa dini zote kukemea vitendo vyovyote vya unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana na kuunga mkono kanuni za msingi za usawa”.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akijibu swali juu ya kipindi hiki kigumu,na  jinsi ya kukabiliana na hisia za hofu ambazo zinaenea miongoni mwa watu amesema, ugonjwa wa homa ya mapafu yaani wa  Covid-19 siyo dharura  pekee ya  kiafya ulimwenguni. Kwa kuthibitisha ameongeza katika wiki za hivi karibuni kumekuwa na kuongezeka kwa nadharia za njama na hisia za ukatili. Katika visa vingine, vimewakumba waandishi wa habari, wafanyakazi wa afya au watetezi wa haki za binadamu ambao wamepata shida kwa sababu ya kufanya kazi yao tu.

Tangu mwanzo wa mgogoro huu, amethibitisha kwamba amehimiza mshikamano kati ya jamii na kati ya nchi. “Mwitikio wetu lazima uwe kwa msingi wa haki za binadamu na utu wa binadamu”. Alikaribisha hata  taasisi za elimu kuzingatia uandishi wa habari wa kidijitali, na kuwahimiza wanahabari, hasa kampuni za mawasiliano ya kijamii, kufanya mengi zaidi katika kuripoti na kuondoa ubaguzi wa rangi, maadili machafu au mengine mabaya, sambamba na sheria za kimataifa juu ya haki za binadamu.

Viongozi wa dini wana jukumu muhimu la kuchukua katika kukuza heshima ya pande zote ndani na nje ya jumuiya zao. Wako katika nafasi nzuri ya kuchangamotisha ujumbe sahihi na mbaya na kuhamasisha jamuiya zote kukuza hali halisi isiyo na  vurugu na ubaguzi wa rangi na aina yoyote ya kutovumilia. Amesisitiza Bwana Guterres.

Katibu Mkuu akijibu swali kuhusu wakati ujao bada ya janga amethibitisha kuwa, kuondokana na ugonjwa huo utatoa  fursa ya kwa ajili ya kuongoza ulimwengu kwenye njia salama, yenye afya, endelevu zaidi na ya umoja. Ukosefu wa usawa na mapungufu katika ulinzi wa kijamii ambayo yameibuka kwa uchungu sana itabidi kushughulikiwa. Itakuwa ni fursa pia  kuzingatia wanawake na usawa wa kijinsia ili kusaidia kujenga ujasiri wa mshtuko wa siku zijazo. Kuanza kwa upya lazima kuambatane na hatua za matendo ya utunzaji wa mazingira.

Hapa amekumbusha jinsi alivyo ziomba serikali kuhakikisha kwamba fedha za kufufua uchumi zinatumika kuwekeza katika siku zijazo, na siyo kwa wakati uliopita. “Pesa za walipa kodi zinapaswa kutumiwa kuharakisha uamuaji wa nyanja zote za uchumi wetu na kupendelea uundaji wa kijani. Huu ni wakati wa kutoza ushuru wa makaa ya mawe na kumfanya alipe anaye chafua mazingira kwa uchafuzi wake. Taasisi za kifedha na wawekezaji lazima wazingatie  hatari za hali ya hewa. Mfano wetu unaendelea kuwa malengo ya maendeleo endelevu na Mkataba wa Paris juu ya mabadiliko ya hali ya hewa. Huu ni wakati wa kuamua. Kuwa na msimamo wa kumshinda Covid-19 na kutoka kwenye mgogoro  ili kuweza kujenga ulimwengu ulio bora  kwa kila mtu.

27 May 2020, 09:04