Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Jacqgues Assanvo Ahiwa kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Bouakè, huko Pwani ya Pembe. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Jacqgues Assanvo Ahiwa kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Bouakè, huko Pwani ya Pembe. 

Mh. Pd. Jacques A. Ahiwa: Askofu Msaidizi Jimbo kuu la Bouakè!

Askofu mteule Jacques Assanvo Ahiwa alizaliwa tarehe 6 Januari 1969 huko Kuindjabo, Wilaya ya Abisso, Jimbo Katoliki la Grand Bassam. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 13 Desemba 1997. Tangu wakati huo kama Padre, ametekeleza dhamana na utume wake kama Paroko-usu; Katibu wa Jimbo na Mkurugenzi wa Mashirika ya PMS.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Jacques Assanvo Ahiwa, kutoka Jimbo Katoliki la Grand Bassam kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Bouaké lililoko nchini Pwani ya Pembe. Kabla ya uteuzi huu, alikuwa ni Jaalimu katika Chuo Kikuu cha Strasbourg, kilichoko nchini Ufaransa. Askofu mteule Jacques Assanvo Ahiwa alizaliwa tarehe 6 Januari 1969 huko Kuindjabo, Wilaya ya Abisso, Jimbo Katoliki la Grand Bassam. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 13 Desemba 1997. Tangu wakati huo kama Padre, ametekeleza dhamana na utume wake kama Paroko-usu; Katibu wa Jimbo na Mkurugenzi wa Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa, PMS.

Kuanzia mwaka 2002 hadi mwaka 2004 akatumwa na Jimbo kujiendeleza zaidi katika Taalimungu ya Biblia na hatimaye akajipatia Shahada ya Uzamili toka Chuo Kikuu cha U.C.A.O./U.U.A. Yaani Université Catholique de l’Afrique de l’Ouest. Kati ya Mwaka 2004 hadi mwaka 2011 alijiendeleza zaidi na hatimaye, kujipatia Shahada ya Uzamivu katika Taalimungu ya Biblia. Kati ya Mwaka 2011 hadi mwaka 2018 akateuliwa kuwa ni Makamu wa Askofu, Jimbo Katoliki la Grand Bassam. Na tangu mwaka 2018 hadi kuteuliwa kwake kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Bouaké nchini Pwani ya Pembe, alikuwa ni Jaalimu.

Askofu Mteule
05 May 2020, 13:43