Tafuta

Papa Francisko amedhimisha Misa ya  Jumapili ya Matawi na nyuma yake upo Msalaba kutoka Kanisa la Mtakatifu Marcel mjini Roma. Papa Francisko amedhimisha Misa ya Jumapili ya Matawi na nyuma yake upo Msalaba kutoka Kanisa la Mtakatifu Marcel mjini Roma. 

Wiki Kuu kwa mtazamo wa Msalaba wa Kanisa la Mtakatifu Marcel

Baada ya kuwekwa Msalaba katika sala ya tarehe 27 Machi 2020 katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,msalaba wa miujiza unaoheshimiwa na Waroma unarudi kuwa kiini cha liturujia mbali mbali za kipindi hiki kikuu.

VATICAN NEWS

Wiki Kuu ambayo ni kipindi cha liturujia muhimu sana cha mwaka, imeanza katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro chini ya mtazamo wa Msalaba wa Mtakatifu Marcel, ambao umewekwa katikati  nyuma  kwenye ukuta wa Kanisa Kuu Kuu. Msalaba huo wa miujiza ulinusurika kuchomwa moto kunako mwaka 1519 na ulikuwa unachukuliwa katika maandamano  huku wakiomba Mungu ili asitishe janga la wakati ule. Msalaba huo wa miaka ya zamani ya miatatu umeweza kupitia na kukatisha mara nyingi katika mji wa Roma. Kabla ya leo, mara ya mwisho ilikuwa ni  kwa miaka ishirini iliyopita wakati Mtakatifu Yohane Paulo II alipendelea uletwe katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro katika fursa ya Siku ya msamaha, kwenye fursa ya Jubilei ya miaka 2000.

Papa Francisko kwanza alikuwa ameamua kwwenda na kutembelea Kanisa hilo na kusali mbele ya msalaba huo katika kipindi hiki cha janga na baadaye akapendelea tena uwepo katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa ajili ya ibada ya Statio Orbis, yaani sala ambayo aliiongoza mwenyewe kwa ajili ya kuomba Mungu ili janga hili liishe.

Tarehe 27 Machi kama inavyojulikana mvua ilinyesha. Msalaba huo ukiwa na picha ambapo pamoja na Askofu wa Roma viliweza kutazamwa na mamilioni ya watu waliokuwa wanafuatilia kwa njia ya Televisheni na majukwaa mbambali ya mitandao. Kutokana na kwamba ulikuwa umewekwa mbele ya Kanisa Kuu, uliweza kufikiwa na kunyeshewa na mvua. Hata hivyo kwa jinsi ulivyoweza kuonekana vizuri shukrani katika muonekano wa kiini cha liturujia ya Ibada ya Misa ya Matawi  imeoneshwa wazi msalaba huu  haukuweza kupata madhara makubwa au yenye maana na  badala yake kwa mujibu wa wengine, picha katika msalaba imekuwa kinyume chake. Ukarabati wake baada ya mvua hiyo ulikuwa kidogo sana kwa mujibu wa wataalam wa sanaa ya Majumba ya Makumbusho na kwa makubaliano na Wakuu wengine nchini Italia. Marekebisho hayo yalihusu kuachana kutokana na kubadilishwa sehemu moja kwenda nyingine. Hatua hiyo ndogo ya marekebisho ya sanaa imewezesha kuiweka kuwa salama zaidi,  kwa maana hiyo baada ya maadhimisho ya Pasaka msalaba huo utaweza kurudishwa mahali pake katika Kanisa la Mtakatifu Marcel mjini Roma.

Katika tamaduni ya kikristo, sanaa na uzuri vimekuwa daima vinapata nafasi msingi, kwa ajili ya kujikita kwa kina ndani ya fumbo la maadhimisho ya liturujia na katika utambuzi wa Maandiko Matakatifu. Msalaba huo ni kazi ya sanaa kubwa na ambayo iliyozunguka katika historia ya Mji wa Milele ukiwa umebeba uchungu, sala, matumaini na ibada za watu. Msalaba huo umekuwa daima sehemu moja wapo ya kufikia na kuukimbilia kwa namna ye pekee katika majanga ya maisha ya watu wa Roma katika karne zilizopita. Kwa maana hiyo uwepo wake katika uwanja wa Mtakatifu Petro  siku ile tarehe 27 Machi 2020 na sasa ndani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro katika ibada Kuu za kipindi cha Pasaka ni kuonyesha kwa mara nyingine umuhimu wake wa kina. Watu wengi duniani, katika kipindi hiki cha uchungu na mamia elfu ya watu waathirika wa janga wote kwa haraka wanaunganishwa katika msalaba.

05 April 2020, 14:00